• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WANAWAKE WANA NAFASI KUBWA KUINUKA KIUCHUMI KUPITIA SEKTA YA MADINI-DKT. GWAJIMA

Imewekwa: March 3rd, 2025

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, amewahimiza wanawake kushiriki kwa wingi katika sekta ya madini kama njia ya kuwawezesha kiuchumi na kuchochea maendeleo ya Taifa. 

Akizungumza katika Kongamano la Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani la Kanda ya Ziwa lililofanyika tarehe 02 Machi, 2025 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Ushirombo, Wilaya ya Bukombe, mkoani Geita, Dkt. Gwajima amesema wanawake wanachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa nchi kupitia sekta hiyo na wanapaswa kupata fursa sawa za kumiliki na kuendeleza shughuli zao. 

“Ni ukweli usiopingika kuwa wanawake wanachangia pakubwa katika uchumi wa nchi kupitia sekta ya madini. Hivyo, ni muhimu kuhakikisha wanapata fursa sawa za kumiliki na kuendeleza shughuli zao ili kujipatia kipato na kukuza uchumi wa familia na jamii kwa ujumla” amesema Dkt. Gwajima. 

Amefafanua kuwa mada kuu ya kongamano hilo ni Ushiriki na Nafasi ya Mwanamke kwenye Maendeleo ya Sekta ya Madini ikilenga kuhamasisha wanawake kushiriki zaidi katika sekta hiyo, hususan kwa Kanda ya Ziwa, ambapo tayari Mkoa wa Geita una vikundi 43 vya wanawake vinavyomiliki leseni za uchimbaji madini na vikundi vingine 20 vilivyopatiwa vitalu vya madini. 

Katika kongamano hilo, Dkt. Gwajima ameeleza changamoto zinazowakumba wanawake wanaojihusisha na uchimbaji na uchakataji wa madini, ikiwemo upungufu wa vifaa vya kuchakata madini, mitaji pamoja na elimu.

 Dkt Gwajima ameahidi kuzitatua changamoto hizo kwa kuziunganisha na zingine zote kutoka Kanda zote saba za makongamano Ili, kushirikisha sekta zote husika kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na wakuu wa mikoa husika.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martine Shigela, amemshukuru Waziri Gwajima kwa kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika sekta ya madini na kusikiliza changamoto zao.

Shigela ameahidi kuhakikisha changamoto zote zilizotolewa katika kongamano hilo zinakusanywa na kufanyiwa kazi ili kutoa suluhisho la kudumu kwa wanawake wa Kanda ya Ziwa.


Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa