• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Baraza la Wahe.Madiwani Latoa Zawadi kwa Shule zilizofanya vizuri.

Imewekwa: May 20th, 2022

Baraza la Wahe. Madiwani  limetoa vyeti vya pongezi  kwa shule za serikali na binafsi zilizofanya vizuri katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne 2021 pamoja na zawadi kwa walimu waliofaulisha masomo yao kwa asilimia 100.

Vyeti vya pongezi hizo pamoja na zawadi vimetolewa tarehe 18 Mei, 2022 katika  Mkutano wa Baraza la Madiwani la kupitia na kujadili taarifa za robo ya tatu ( Januari- Machi) kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Leokadia Kasase  amewashukuru sana walimu kwa kuinua kiwango cha elimu.

" Walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mmetuheshimisha sana. Tunawashukuru sana kwa kuinua Taaluma katika wilaya yetu na muendelee kuwa na moyo huo huo wa kizalendo wa kujitolea katika masuala ya ufundishaji na ujifunzaji."

Aidha ameipongeza shule ya sekondari Bulega kwa kuongoza kiwilaya katika matokeo ya kidato cha nne katika kundi la shule za serikali.

" Kipekee naipongeza shule ya sekondari Bulega kwani shule hii kwa miaka miwili mfululizo ilikuwa  inakuwa ya mwisho na sasa mmeibuka kidedea. Hongereni sana. "

Naye Diwani wa Kata ya Bulega Mhe.Erick Kagoma ameishukuru serikali kwa kupeleka umeme katika shule yake kwani wanafunzi wamekuwa na tabia ya kujisomea nyakati za usiku na kupelekea kufanya vizuri katika mitihani.

"Tunaishukuru sana serikali kwa kutuletea umeme katika shule yetu ya sekondari Bulega ambao umehamsha moyo wa wanafunzi kujisomea nyakati za usiku na kupandisha ufaulu katika shule yetu."

Shule ya wavulana ya Seminari ya Queen of Apostle katika shule za sekondari binafsi iliongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kiwilaya, kimkoa na Kitaifa katika kundi la watahiniwa chini ya wanafunzi 40 huku ikifuatiwa na shule ya binafsi Emink ambayo ilishika nafasi ya pili kiwilaya.

Kwa upande wa shule za serikali, shule ya sekondari Bulega ilishika nafasi ya kwanza kiwilaya na ikifuatiwa na shule ya sekondari Lyambamgongo na iliyoshika nafasi ya tatu ni shule ya sekondari Musasa.

Vilevile katika Matokea ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne 2021 Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe iliongoza kimkoa kwa kushika nafasi ya kwanza.

https://www.instagram.com/p/CdwiSFXIWMq/?igshid=MDJmNzVkMjY=


 


Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa