• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

TUNAISHUKURU TIMU YA MADAKTARI BINGWA KWA KUJA KUTUONGEZEA NGUVU. DC - MURAGILI

Imewekwa: November 15th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Paskasi Muragili ameishukuru timu ya Madaktari Bigwa wa Rais Samia  kwa kutoa huduma za Mkoba za Kibingwa na Ubingwa Bobezi pamoja na kuwaongezea  nguvu Madakta wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe.

" Tunawashukuru sana kwa huduma za kibingwa mnazoendelea kutoa  katika Wilaya yetu kwa kufanya hivyo mmeweza kutuongezea ujuzi ambao utapelekea kupunguza huduma za rufaa."

Hayo ameyasema leo tarehe 15 Novemba, 2024 wakati wa hafla ya hitimisho la kliniki ya Madaktari Bingwa iliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Bukombe.

Aidha amemshukuru Mhe.Rais kwa kuhakikisha huduma  za kibingwa zinawafikia wananchi katika maeneo wanayoishi.

"Tunamshukuru sana Rais kwa kuwafikishia wananchi huduma karibu na maeneo yao kwani hapo zamani walikuwa wanazifuata huduma hizi katika Hospitari za rufaa."

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Lutengano Mwalwiba amesema ujuo wa Madaktari Bingwa umekuwa ni fulsa kubwa katika Wilaya  kwani wameweza kubadilishana uzoefu na Madaktari wetu kwa kuwapa ujuzi pamoja na uzoefu wa kutosha.

Aidha Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Dr.Deograsia Mkapa ameishukuru Serikali kwa kuiwezesha Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kupata kupata Vifaa tiba vya kisasa ambavyo vimewasaidia Madaktari Bingwa kutoa huduma za kibingwa.

Akiongea kwa niaba ya wagonjwa Eva Kapera Mkazi wa Mtaa wa Kitangili Wilayani Bukombe, ameishukuru Serikali kwa kusogeza huduma karibu kwani imempunguzia gharama za kwenda kufuata huduma KCMC na sasa amezipata Hospitali ya Wilaya ya Bukombe.

Kuanzia tarehe 11-15 Novemba, 2024 jumla ya wagonjwa 342 wamepata huduma za kibingwa kutoka kwa madaktari wa Magonjwa ya Upasuaji na mfumo wa njia ya mkojo, Magonjwa ya ndani ( Kisukari,Ini, figi, shinikizo la damu),  Magonjwa ya Wanawake na Ukunga, Magonjwa ya Watoto na Watoto Wachanga, Magonjwa ya Kinywa na Meno na Magonjwa ya Mifupa na ajali.



Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa