• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WAJUMBE WA KAMATI YA HUDUMA ZA MIKOPO YA KATA WATAKIWA KUTENDA HAKI

Imewekwa: October 9th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Paskasi Muragili amewataka wajumbe wa kamati ya huduma ya Mikopo ya Kata kuhakikisha watenda haki wakati wa uidhinishaji wa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye ulemavu.

"Mtakapokuwa waaminifu, waaadilifu na watenda haki tunaamini hakutotokea  malalamiko yoyote wakati wa zoezi zima la utoaji mikopo na urejeshaji."

Muragili ameyasema hayo tarehe 09 Oktoba, 2024 wakati wa mafunzo ya wajumbe wa kamati ya Mikopo ya Kata ya kuimarisha uelewa juu ya kanuni na mwongozo mpya za utoaji wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri.

Aidha amewataka wajumbe hao kufanya kazi kwa bidii ili zoezi liweze kuwa na mafanikio makubwa kwa  kufuata kanuni  za mwongozo mpya ambao unatatua changamoto zote za awali.

Akiongea wakati wa kikao hicho kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Melania Kwai ambaye ndiye Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii alisema, wajumbe wa kamati ya huduma ya Mikopo ngazi ya kata ni Watendaji wa Kata, Maafisa Maendeleo ya Jamii Kata, Maafisa Ustawi wa Jamii Kata, Maafisa Ugani wa Kata, Maafisa Elimu Kata, Watendaji wa Vijiji na Polisi Kata na jukumu lao la Msingi nikuhakikisha uwazi, ufanisi na uwajibikaji katika mchakato wa utoaji mikopo.

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Uyovu  Marco Nsolo akiongea kwa niaba ya washiriki wa mafunzo, ameishukuru serikali kwa kuwezesha mafunzo hayo kwani wataweza kufanya tathmini ya awali ya maombi ya mikopo yaliyowasilishwa, kutembelea vikundi vilivyoomba mikopo,  kuaanda taarifa ya hali halisi ya vikundi na kuwasilisha katika kamati ya mikopo ya halmashauri.

Sambamba na mafunzo hayo washiriki walikula kiapo cha kuepuka mgongano wa maslahi

Kwa mwaka wa fedha 2024/2025 serikali ilitangaza kurudisha mikopo ya asilimia 10 kwa kanuni na miongozo mipya ziitwazo Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu za mwaka 2024 kwa ajili ya kutatua changamoto za nyuma zilikuwa zimejitokeza.


Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa