• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wakuu wa Wilaya Watakiwa Kutatua Changamoto ya Upungufu wa Vyumba vya Madarasa.

Imewekwa: June 22nd, 2021

 Mkuu wa Mkoa wa Geita amewataka Wakuu wa Wilaya kwenda kusimamia kwa karibu Ujenzi unaoendelea wa Miradi ya maendeleo yakiwemo Madarasa ili kutatua changamoto hiyo inayozikabili Halmashauri za Mkoa huo kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi.

Akizungumza kwenye Hafla ya kuwakaribisha Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Geita leo tarehe 22 Juni, 2021 Mhe. Senyamule amewataka viongozi hao kutembelea shule na kuweka mazingira ya kuwapongea wanafunzi kwenye shule tisa ambazo mwezi Julai mwaka huu zitawapokea wanafunzi wa kidato cha tano.

"Shule mpya tisa zinaanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano mwezi Julai ,tukahakikishe mahitaji yote muhimu kwenye shule hizo yanakamilika kabla ya ya shule hizo kufunguliwa," amesema Mkuu wa Mkoa.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amezipongeza Halmashauri zilizofanya vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa Fedha 2020/21 ikiongozwa na Geita iliyokusanya kwa 125%, Nyang'hwale 119%, Mbogwe 116% na Geita Mji 101% na amezitaka Halmashauri za Chato iliyokusanya kwa 92% na Bukombe iliyofikia 79% kuhakikisha ifikapo Juni 30 wawe wamefika asilimia 100.

Wakitoa salamu katika nyakati tofauti, Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya wameahidi kufanya kazi kwa bidii na wameahidi ushirikiano wa kutosha kwa viongozi na watendaji ngazi zote ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Katika wakati mwingine, Afisa Lishe wa Mkoa wa Geita Riziki Mbilinyi amewasilishwa mada ya Tathmini ya Mkataba wa Lishe iliyoonesha Udumavu kwa watoto Mkoa wa Geita ni wa 38.9% zaidi ya 31.8% ya Kitaifa ambapo amesema pamoja na mambo mengine hali hiyo imechangiwa na kutoweka bajeti ya kutosha kwenye masuala ya Lishe na Ukosefu Chakula dawa kwa ajili ya matibabu ya Magonjwa ya Utapiamlo.

Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Geita kuhakikisha wanatenga Fedha za Lishe kwenye bajeti za Halmashauri zao ili kufanikisha adhma ya kuisaidia jamii.

 "Suala la kutenga Fedha za Lishe na kutoa fesha hizo lisiwe la hiari tufanye hivyo na Maafisa Lishe Tutumie maarifa yetu kuhakikisha tunaelimisha jamii kuhusiana na masuala ya Lishe bila kuchoka," amesema.

Vilevile, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Michael Mashala ametoa tahadhari ya Ugonjwa wa Uviko 19 (Covid 19) na kusema Wananchi wasipuuze ugonjwa huo kutokana na kuwepo kwa viashiria vya kutokea kwa wimbi la tatu la athari za ugonjwa huo nchini kutokana na uwepo wa virusi anuai vya kirusi kipya.Kunawa mikono Mara kwa Mara kwa Maji tiririka na sabuni, Uvaaji sahihi wa Barakoa Safi na Salama, Kuepuka Msongamano usio wa lazima na kukaa umbali wa mita moja na zaidi, Kufanya Mazoezi kulingana na Afya ya Mtu husika, Kuzingatia Lishe Bora, Uzito uliopitiliza na Wenye Magonjwa ya kudumu ni miongoni mwa makundi yaliyobainishwa kuhakikisha wanachukua tahadhari ya ugonjwa wa Uviko 19.

"Tukaongeze nguvu zaidi, maarifa zaidi na tukaone namna ya kuweka mkazo kwenye suala la Lishe na tulione kuwa ni miongoni mwa Mambo ya ya Msingi kwenye Ujenzi wa taifa letu, pia tukatoe Elimu na kutenga bajeti kwenye masuala ya Lishe na kwa hekma twende tukaweke mikakati ambayo haijengi hofu lakini tukajikinge na maambukizi ya ugonjwa kwa Uviko 19 (Covid 19)" Amesisitiza Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Geita kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wakati akihitimisha hafla hiyo.





Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa