• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi 51, 880 Kunufaika na Miradi ya Maji Bukombe

Imewekwa: July 5th, 2022


Jumla ya wananchi 51,880 katika vijiji 11 mbioni kunufaika na miradi 8 ya Maji yenye thamani ya kiasi cha shilingi Bilioni 4.1 sawa na asilimia 108 ya Bajeti ya mwaka 2021/2022 inayoendelea kutekelezwa wilayani Bukombe.

Yamebainishwa hayo tarehe Julai 05, 2022 na Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) Jemas Benny wakati wa ziara ya  kutembelea na kukagua miradi ya maji iliyopokea fedha kupitia programu ya Malipo kulingana na Matokeo pamoja na Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko - 19.

"Tumejipanga kusimamia miradi ya maji na kuhakikisha inakamilika kwa muda uliopangwa hali ambayo itawasaidia wananchi kupata huduma za maji safi na salama katika maeneo wanayoishi." Benny amefafanua.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanaitunza na kuilinda miundombinu hiyo ili huduma ya maji safi na salama iwe endelevu.

"Wananchi wenzangu tuhakikishe tunatunza miundombinu ya maji inayojengwa vilevile kutunza vyanzo vya maji kwa kutokufanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita 60 ya vyanzo hivyo," amesema Benny.

Naye, Vumilia John mkaazi wa kijiji cha Bugelenga ameishukuru serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa kuwasogezea  huduma ya maji katika maeneo yao.

"Tunaishukuru sana serikali kwa kutuletea huduma ya maji safi  kwani hapo nyuma tulikua tukitumia maji ambayo siyo safi na salama lakini kupitia miradi hii naamini tutatumia maji yaliyo safi na salama."

Miradi yote ya maji inayotekelezwa katika halmashauri ya Wilaya ya Bukombe inahusisha ujenzi wa 'Power House', uunganishaji wa umeme wa gridi na ufungaji wa pampu ya kusukuma maji, ujenzi wa Matanki pamoja na ujenzi wa vituo 57 vya kuchotea maji.

Vijiji vinavyonufaika na miradi hiyo ya maji ni pamoja na kijiji cha Bugelenga, Katome, Ihako, Namsega, Msangila, Kazilamyaye, Namonge, Nasiluluma, Kanebwa na mtaa wa Butambala.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa