• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi wa Kijiji cha Shibingo, Bulangwa, Ikalanga, kiziba na Nasiluluma watakiwa kushiriki utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi.

Imewekwa: April 11th, 2022

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe Paul Cheyo amewataka wananchi wa kijiji cha Shibingo, Bulangwa, Ikalanga, kiziba na Nasiluluma kuhakikisha  wanashiriki katika utekelezaji wa miradi ya  ujenzi ya kuondoa umaskini kupitia mpango wa TASAF.

"Miradi yetu ili iweze kuleta tija  inategemea  ushiriki wetu sisi wananchi katika  kujitolea nguvu zetu kama vile kuchimba msingi, kuchota maji, kusogeza mawe na hata mchanga.

"Hayo ameyasema tarehe 9 April, 2022 kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Said Nkumba wakati wa zoezi la uzinduzi wa  miradi hiyo.

Vile vile Cheyo amezitaka kamati za usimamizi wa mradi  (CMC)  kuhakikisha wanasimamia mradi kwa umakini mkubwa na kwa viwango ambavyo serikali inatarajia.

Naye Mratibu wa TASAF Prisca Lyimo amesema Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ilipokea kiasi cha  shilingi Milioni 422 kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ofisi moja ya walimu na matundu sita ya vyoo kwa kila shule katika shule ya msingi Ikalanga, Bulangwa na shibingo. 

Na Ujenzi wa Zahanati, matundu manne ya vyoo na kichomea Taka kwa kila kijiji katika kijiji cha Nasiluluma na kiziba.

Kwa upande wake Neema kiziba Athumani mwananchi wa kijiji cha  kiziba ameishukuru serikali kwa kuwasogezea huduma ya afya karibu kwani walikuwa wanatembea umbali mrefu kwenda kupata huduma hiyo katika kituo cha Afya Ushirombo.

Naye Diwani wa Kata ya Bulangwa ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mhe. Yusuph Mohamed Yusuph amesema wananchi wa kata yake wameupokea mradi na wameahidi kuutekeleza.

"Sisi wananchi wa Kata ya Bulangwa tupo tayari kushirikiana na serikali kwa ajili ya kutekeleza mradi kwani mradi huu utasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani katika kata yetu."

Miradi ya ujenzi ya kuondoa umaskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kupitia mpango wa TASAF III awamu ya pili inatekelezwa chini ya ufadhili wa Jumuiya ya nchi zinazozalisha Mafuta Duniani (OPEC).

MWISHO




Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC MURAGILI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE ROBO YA TATU (Januari-Machi 2024/2025)

    May 08, 2025
  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkutano wa baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya 3 kwa mwaka 2024/2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa