• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

NMB Bukombe yachangia mabati 185 na kompyuta 7

Imewekwa: January 30th, 2019

NMB Bukombe imekabidhi mabati 185 yenye  thamani ya shilingi Million 5 kwa shule ya sekondari Ushirombo na kompyuta saba kwa shule ya sekondari Katente tarehe 29 Januari, 2019 ikiwa ni kuhakikisha jamii inafaidika kutokana na faida inayopatikana kutoka kwa wateja wanaotumia benki hiyo.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Said Nkumba ameishukuru NMB  kwa ufadhili walioutoa kwa shule hizo mbili. Pia amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kuhakikisha anasimamia ukamilishaji wa miundombinu hiyo ili ifikapo mwishoni mwa mwezi wa pili mwaka 2019 wanafunzi waweze kuyatumia madarasa hayo.

Aidha Meneja wa NMB Kahama Ndg. Richard Kirenga kwa niaba ya Menaja wa NMB Kanda ya Magharibi alitoa shukrani zake kwa uongozi wa Wilaya ya Bukombe  pamoja na uongozi wa shule ya sekodari Ushirombo na Katente kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha shule hizi zinapata madarasa bora pamoja na vifaa vya KITEHAMA kwa ajili ya ufundishaji na ujifunzaji ili kuimarisha elimu na kuwa mfano bora hapa nchini.

Ndg. Richard aliendelea kusema “katika kuhakikisha tunachangia maendeleo kwa wananchi NMB kwa mwaka 2019 imetenga zaidi ya shilling bilioni 1 kwa ajili ya sekta ya afya na elimu kwani vifaa vya afya na elimu vimekuwa ni changamoto kubwa hapa nchi”.

Naye Meneja wa NMB Bukombe Ndg George Fundi alisema “sisi kama NMB tulipopata maombi yenu tulifarijika na kuamua mara moja kuja kushirikiana na ninyi na kuwa chachu ya maendeleo kwani kupitia jamii NMB imekukuwa benki kubwa kuliko benki yoyote hapa nchini”.

Aidha Diwana wa kata ya Bulagwa  Mhe. Yusuph Mohamed ameahidi kuhakikisha wanaezeka majengo hayo mapema iwezekanavyo ili wanafunzi waweze kutumia miundombinu hiyo inayojengwa kwa kutumia nguvu za wananchi pamoja na fedha za mradi wa P4R (lipa kulingana na matokeo) shillinig milioni 8 zilizobaki baada ya mradi huo kukamilika.

Akihitimisha hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Ndg. Dionis Muyinga aliwaomba wazazi kuhakikisha wanashiriki katika kuchangia shughuli za maendeleo ili Benki ya NMB iendelee kuunga mkono shughuli za serikali. ”NMB imeonyesha njia sie tunatakiwa tutangulie mbele zaidi ili wao waendelee kutuunga mkono”.


Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Said Nkumba akiongea wakati wa hafla  ya kukabidhi mabati na kompyuta

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Said Nkumba akikabidhiwa  kompyuta na uongozi wa NMB


Meneja wa Banki ya NMB Kahama Ndg. Richard Kirenga kwa niaba ya Menaja wa Benki Kanda ya Magharibi akizungumza mbele ya wageni waalikwa

Vyumba 3 vya madarasa na ofisi 1 ya walimu  Vitakavyopauliwa kwa mabati yaliyotolewa na Benki ya NMB katika shule ya sekondari Ushirombo 

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC MURAGILI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE ROBO YA TATU (Januari-Machi 2024/2025)

    May 08, 2025
  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkutano wa baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya 3 kwa mwaka 2024/2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa