• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

BILIONI 22 KUJENGA SOKO NA STENDI USHIROMBO-KATIMBA

Imewekwa: July 31st, 2024

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amesema serikali imetenga shilingi bilioni 22 kwaajili ya ujenzi wa soko na stendi ya mabasi ya kisasa katika eneo la Ushirombo Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe , mkoani Geita.

Kati ya fedha hizo, Sh bilioni 15.89 zitatumika katika ujenzi wa soko la kisasa na Sh bilioni 6.29 zitatumika kwaajili ya ujenzi wa stendi ambapo Serikali imetoa Sh bilioni 1 kama malipo ya awali ya utekelezaji wa miradi hiyo inayotarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2024/2025.

Akizungumza na wananchi wa Ushirombo Julai 28,2024 Wilayani Bukombe mkoani Geita , Mhe.Katimba amesema ujenzi wa soko hilo unaenda sambamba na mahitaji ya kipindi cha sasa.

Amesema soko la sasa uwezo wake ni vibanda vinavyoweza kubeba wafanyabiashara 734 ambapo wenye vibanda halali ni 534 na wasio na vibanda ni 200.

Katimba amesema kuwa Serikali inawekeza Sh bilioni 15.89 kwenye ujenzi wa soko la kisasa litakalokuwa na mabanda kwaajili ya kutosheleza wafanyabiashara 1,301.

“Ndugu zangu hii ni baraka kubwa sana kwa kuwa uwezo wa soko utaongezeka , wafanyabiashara wenye vibanda ambao kwasasa wako 534 lakini soko likiboreshwa wataongezeka hadi kufikia wafanyabiashara 1,301.”

Amesema kwamba uwekezaji huo mkubwa hautawanufaisha wafanyabiashara peke yao bali utasaidia kuongeza mapato ya halmashauri ambapo awali halmashauri ilikuwa ikikusanya kiasi cha shilingi milioni 51.3 kwa mwaka lakini soko likijengwa mapato yataongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 2.2 kwa mwaka.

kwa upande wa mradi wa stendi eneo la Ushirombo, Katimba amesema kuwa kwa sasa stendi hiyo ina uwezo wa kupokea mabasi 50 kwa siku lakini baada ya kujengwa itakuwa na uwezo wa kupokea mabasi yasiyopungua 210 kwa siku.

Aidha ameongeza kuwa baada ya ujenzi wa stendi kukamilika mapato yataongezeka kutoka Sh milioni 155 kwa mwaka hadi kufikia Sh bilioni 1.4 kwa mwaka.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa