• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi wilaya ya Bukombe wang'arisha Mwenge wa Uhuru 2018

Imewekwa: April 6th, 2018

Wananchi wilaya ya Bukombe wamekuwa wachangiaji wakubwa wa maendeleo katika sekta mbalimbali, katika mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya kisasa vya madarasa shule ya sekondari  Ushirombo vyenye thamani ya fedha za kitanzania Milioni 56.1  ambavyo vimefunguliwa rasmi leo na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru na Ndugu Charles Francis Kabeho huku wananchi wakiwa wamechangia  Milioni 3.24.

Pia ametembelea matengenezo ya barabara za ushirombo mjini zenye urefu wa km 10.5 ukiusisha ujenzi wa makaravati 2 kati ya 8 pamoja na mtaro wa maji mmoja, matengenezo haya yameanza rasmi tarehe 12.02.2018 yatakamilika tarehe 11.08.2018 kwa gharama shilingi za Kitanzania Milioni 275.4.

Ndugu Kabeho amezindua mradi wa maji kijiji cha ikuzi kitendo ambacho kimewarahisishia wakazi takribani 4500 wa kijiji hicho kupata maji kiurahisi ukilinganisha na hapo awali walipokuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji. Mradi huo wenye vituo tisa vya kutolea maji umegharimu zadi ya  Milioni 305.

Katika uzinduzi huo, baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ikuzi Consolatha John na Kibitz Mila wameshukuru serikali kwa kuleta mradi huu kwani umeondoa adha ya kutafuta maji umbali mrefu na kupunguza homa za matumbo.

Pia kiongozi wa mbio za mwenge amekabidhi hati kwa kikundi cha vijana wajasiriamalii BORA FOOD  ambacho kinamiliki kiwanda kidogo cha uchakataji nafaka. katibu wa kikundi hicho Bwana Wisdom Mola kwa niaba ya wanakikundi wenzake amesema wamefurahi na wameishukuru serikali kwa kutambua jitihada zao za kujikwamua kiuchumi na kuendeleza dhana ya Tanzania ya viwanda na kauli mbiu ya Mhe Rais ya hapa kazi tu, pia ametoa changamoto ya ukosefu wa soko la uhakika na nishati ya kutosha.

Ndugu Charles Francis Kabeho ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa miundo  mbinu mbali mbali yenye thamani ya Tsh ml 400, kama kliniki ya baba mama na mtoto, wodi ya watoto, jengo la maabara na nyumba ya mtumishi katika kituo cha afya Uyovu.

Katika eneo la mkesha wa Mwenge wa Uhuru kijiji cha Lyobahika, kiongozi wa Mbio za Mwenge ametoa wito kwa wananchi wa Bukombe kutunza na kuthamini miundombinu ya miraji inayoletwa na serikali kwa manufaa ya maendeleo ya wananchi, pia amesisitiza wazazi kuhakikisha watoto wanaenda shule kwani sera ya elimu bure intatoa nafasi kwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule aende shule, kama kauli mbiu inavyosema "Elimu ni ufunguo wa maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu" alisema Kabeho.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndugu Charles Francis Kabeho akikata utepe kuashiria utayari wa kufungua Jengo jipya la Madarasa Shule ya sekondari Ushirombo.

Jengo la kisasa la Vyumba Vitatu vya Madarasa vilivyofunguliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Katika Shule ya Sekondari Ushirombo kata ya Bulangwa.



Mkuu wa wilaya ya Bukombe mhe.Josephat Maganga akipokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe mhe.Martha Mkupasi.

Dr Irene Mukerebe akisoma taarifa ya mapambano dhidi ya malaria katika mradi wa kugawa vyandarua kwa wamama wajawazito na watoto.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu Charles Francis Kabeho akimpatia mama mwenye mtoto wa meiji 2 chandarua.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 Ndugu Charles Francis Kabeho akimtwisha ndoo ya Maji mmoja wa watumia maji kijiji cha Ikuzi.

Tenki la Maji linalopokea Maji kutoka Chanzo kikuu na kusambaza kwa Vituo tisa vinavyotoa huduma ya Maji kwa Wananchi.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge amemkabidhi Katibu wa kikundi cha Viana Wajasiliamli Bwn.Wisdom Mola hati ya pongezi kwa kuwa na kiwanda kidogo cha uzalishaji nafaka.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa