• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

“Bukombe moja tusafiri patoja" DC Nkumba

Imewekwa: August 27th, 2018

Mkuu wa wilaya ya Bukombe Mhe.Said Nkumba amefanya kikao kazi cha kuhimiza na kuboresha utendaji kazi ili kuwaletea wananchi wa Bukombe maendeleo, kikao hicho kimejumuisha Wenyeviti wa Vitongoji ,Vijiji ,Maafisa Ugani, Watendaji wa Vijij na Kata wa Tarafa ya Siloka  inayoundwa na kata za  Busonzo, Namonge, Runzewe Mashariki,  Runzewe Magharibi na kata ya Uyovu hivi leo.

Katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya amewataka Viongozi wa Vijiji na Vitongoji kufanya kazi za maendeleo na sio kuendelea na mambo ya siasa katika kipindi cha kuleta Maendeleo, na washirikiane kuleta maendeleo na sio mambo ya kusema tukifanya hiki tutawapa chama fulani sifa,”shughuli za maendeleo ndani ya Bukombe hakuna mambo ya chama, kama unataka mambo ya chama subirini 2020” alisema Nkumba.

Pia Mhe.Nkumba amesisitiza sekta zote zinazotoa huduma kwa wananchi kuzingatia maadili na uwajibikaji kwa kuongea lugha nzuri kwa wananchi ambao ndio wateja wetu, uwajibikaji wa kila mtumishi katika eneo lake hususani watumishi wa afya,Elimu na makao makuu ya Halmashauri, pia vitendo vya rushwa kwenye Zahanati,Vituo vya Afya na Hospital ya wilaya  ni marufuku.

Mhe.Nkumba amewatangazia vita walimu wanaofumbia macho suala la utoro na mimba mashuleni, na wale walimu wanaotembea na wanafunzi , na ametoa rai kwa wazazi ambao wanamaliza kesi za mimba na walimu au wenyeviti wa vijiji au vitongoji kuacha mara moja, kwani kwa kufanya hivyo wanarudisha maendeleo ya watoto ambao ni Taifa la kesho la kuwakwamua wazazi kiuchumi.

Mkuu wa wilaya pia amesikiliza kero mabalimbali na kupatiwa majibu papo kwa papo ikiwemo kero ya umeme kutofika sehemu zote za vijiji,ambapo Mkurugenzi mtendaji aliwaambia alifuatilia suala hili hadi ngazi ya mkoa ofisi za Tanesco na aliambiwa umeme utawekwa mjini na kusambazwa vijiji vyote mpaka kufikia  mwaka 2022.

Na amesisitiza Afisa Ardhi na Mwanasheria kutatua kero za migogoro ya ardhi haraka sana kama ipo ndani ya uwezo wao na zilizo nje ya uwezo ziandikiwe taarifa na kupelekwa ngazi inayohusika.

Mkuu wa  wilaya ya Bukombe Mhe.Said Nkumba akiwasisitiza wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na watendaji wa kata na vijiji pamoja na Maafisa ugani kutekeleza Ilani ya Chama cha mapinduzi.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Said Nkumba akisisitiza uwajibikaji katika mkutano huo.

Ndugu Benedicto Mwenyekiti wa kijiji Kabuhima akitoa malalamiko yake.

Maafisa ugani wa kata ya Uyovu wakipokea maelekezo ya kuwa na Shamba darasa la kuwafundishia Wananchi.

Bi.Habiba akitoa kero yake kwa Mkuu wa Wilaya katika kikao hicho.

Wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji, watendaji wa kata na kijiji waliojitokeza Kwenye mkutano huo.

Wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji, watendaji wa kata na kijiji waliojitokeza Kwenye mkutano huo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri akiijibu malalamiko mbalimbali ya wananchi.

Afisa Kilimo wa Wilaya Bwana Joseph Machibya akijibu Maswali ya Pamba.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa