• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Bulangwa Wasogezewa Huduma za Afya

Imewekwa: June 10th, 2021

Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Sekretarieti Mkoa wa Geita imefurahishwa na Matumizi ya Tshs. Milioni 63 zilizojenga Wodi ya Wagonjwa wa Nje, Wodi ya Mama na Mtoto, Nyumba ya Watumishi, Wodi ya Wazazi na Vyoo vya Wagonjwa na Watumishi kwenye Zahanati ya Bulangwa wilayani Bukombe ambayo mwaka 2020 ilianza kutoa huduma na kusaidia kupunguza Vifa vitokanavyo na  Uzazi.Hayo yamejidhihirisha leo tarehe 10 Juni, 2021 baada ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Alhadji Said Kalidushi kukagua zahanati hiyo na kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kwakutumia fedha vizuri na kufanikisha kutekeleza Mradi kwa ufanisi mkubwa ambapo ameita juhudi hizo kuwa ni za kizalendo.

Wakati huohuo Kamati ya Siasa ya Mkoa imeridhishwa na jinsi Halmashauri hiyo inavyojali makundi ya vijana, wanawake na walemavu kwa kuwapatia mikopo inayosaidia kuendesha Shughuli mbalimbali za ujasiriamali kwani ilipotembelea Kikundi cha Amani Maseremala kilichopo Masonga-Runzewe Mashariki kilichoanzishwa Julai 2019 Katibu wa kikundi hicho alielezea kuwa wamekopeshwa Milioni 4 kwa ajili ya kununua vitendea kazi vya kisasa ili watengeneze samani za kimataifa.

Awali, Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Said Nkumba amefafanua kuwa Wilaya ya Bukombe inawahudumia wananchi wote bila kujali tofauti za dini na vyama na kwamba Wilaya hiyo inasimamia uvunaji wa mbao wanazotumia wajasiriamali hao ili zivunwe kwa kufuata taratibu na Sheria pasipo  kuharibu mazingira kwa kukata misitu.

Awali, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Alhadji Said Kalidushi ametoa rai kwa viongozi wa Wilaya hiyo kurekebisha Mapungufu yaliyojitokeza kwenye  Miundombinu ya machinjio ya Mwalo hasa kukosekana kwa nishati ya Umeme, Choo na Mazingira ya Usafi wa machinjio hayo ili eneo liwe nadhifu na kwa kipindi cha ukarabati kamati hiyo imeelekeza kufungwa kwa muda kwa machinjio hayo ambapo watumie machinjio ya Katente wakati wa mpito.

Baadae, Kamati hiyo ilifika kwenye Mradi wa Ukamilishaji wa Ujenzi wa Nyumba 10 za watumishi wa Halmashauri ya Bukombe ambao mwaka 2012/13 serikali ilitoa Tshs. Milioni 30 kwa kila Nyumba na baadaye ilionekana kuwa fedha hizo kuwa pungufu kwani kila Nyumba ina gharama za Milioni 60 ya ujenzi. Mwaka 2021/22 serikali imeomba fedha kutoka serikali kuu kukamilisha ujenzi wa Nyumba hizo.

Vilevile, Mwenyekiti wa CCM Mkoa amewapongeza Wakala ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini  (RUWASA) na Kamati ya jumuiya ya watumia Maji kwa kazi nzuri na Usimamizi mzuri wa Mradi wa Maji Buganzu-Uyovu ambapo kwa muda mfupi tayari wameshakusanya zaidi ya Tshs. Milioni 43. Aidha, Mradi huo umegharimu Tshs. Milioni 158 na zaidi ya watu 2000 wananufaika 

Bi. Rahel Ndegeleke, Katibu wa CCM Mkoa wa Geita ametoa rai kwa TANESCO kumaliza tatizo la Uhaba wa Mita za Umeme  kwa wateja wapya wanaopeleka maombi ya kuunganishwa na huduma za umeme wilayani Bukombe.

Kabla ya Kamati hiyo kuhitimisha ziara wilayani Bukombe , Sauti ya furaha ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita ilisikika tena baada ya kutembelea Mradi wa Ukamilishaji wa kituo cha Afya Namonge-Siloka ambao uliasisiwa na wananchi mwaka 2012 kwa kutoa eneo la hekari 6 na kuanzisha ujenzi ambapo Serikali iliongeza nguvu na kupelekea pamoja na nguvu za wananchi na wadau mbalimbali jumla ya Tshs. Milioni 274 zitatumika kukamilisha.






Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC MURAGILI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE ROBO YA TATU (Januari-Machi 2024/2025)

    May 08, 2025
  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkutano wa baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya 3 kwa mwaka 2024/2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa