• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Chanjo ya Uviko-19(Covid-19) yazinduliwa Geita.

Imewekwa: August 4th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Rosemary Senyamule amewaongoza wananchi wa Mkoa huo kupata Chanjo ya Ugonjwa wa Uviko 19 (Covid 19) leo tarehe 04 Agosti, 2021 kwenye hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa GEDECO mjini Geita.

Akizungumza kwenye Uzinduzi huo Mhe. Mkuu wa Mkoa ameishukuru serikali kwa kuwajali wananchi kwa kuwaletea Chanjo ili kuwakinga na Maradhi hayo yaliyo kwenye wimbi la tatu la maambukizi tangia kuibuka kwa ugonjwa huo mwaka 2019.

Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa wananchi kwenda kupata Chanjo hiyo kuanzia leo siku ya uzinduzi kwenye vituo vilivyobainishwa ambapo kwa Mkoa wa Geita wananchi wapatao elfu 50 watapata Chanjo hiyo kwa awamu ya kwanza kwenye vituo 18 yaani vituo vitatu kwenye kila Wilaya.

"Serikali yangu inajali na inawatakia mema watanzania wote, natoa wito kwa Makundi yote yaliyobainishwa kwa awamu ya kwanza kwenda kupata chanjo hii muhimu", amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Wilson Shimo pamoja na mambo mengine ametoa rai kwa wananchi kufanya mazoezi ya viungo na kuzingatia Lishe Bora kwa kula vyakula vyenye mlo kamili pamoja na vitamini C.

"Tunachokifanya hapa ni kwa maslahi ya Afya zetu, ..twendeni tukapate chanjo kwani pamoja maneno mengi yanayozunguka lakini hili tatizo lipo". amesema Mwinyiheri Baraza, kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa.

Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoriki Tanzania (TEC) na Askofu wa Kanisa katoriki Mkoa wa Geita, Flavian Kasala ametoa pongezi kwa serikali kwa uamuzi wa kuwapatia Chanjo ya Ugonjwa wa Uviko 19 ( Covid 19) na amewasihi wananchi kupata Chanjo ya Ugonjwa ili kulinda Afya zao. "katika awamu hii ya mzunguko wa tatu, tatizo hili limejidhihirisha kuwa ni kubwa sana," amesema.

"Ni nafasi kwa sisi kuonesha Imani kubwa kwenu katika kutusimamia kwani uwepo wenu ni kwa ajili ya Ustawi wa Taifa, kwani utaalamu wa kisayansi na Imani kwa viongozi wetu.Mimi binafsi nakubali kuingia katika Chanjo na natoa wito kila mmoja ajitafakari na aone umuhimu na kupata Chanjo". Askofu Kasala.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Japhet Simeo amebainisha kuwa Chanjo ya ugonjwa wa Uviko 19 (COVID 19) inasaidia kupunguza uwezekano wa mgonjwa kupata dalili kali na hatarishi na inapunguza upotevu wa uhai wa watu.

Aidha, Mganga Mkuu amesema Mkoani Geita jumla ya wananchi laki tatu watapata Chanjo hiyo.

Paul Zahoro

Geita RS.


Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa