• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DAS Bukombe awataka watumishi wa Umma kufanya kazi kwa kuzingatia maadili

Imewekwa: June 12th, 2019

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe, Paul Cheyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya amewataka watumishi wa kituo cha Afya Ushirombo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya Utumishi wa umma ili kujiepusha na vitendo vya rushwa. 

Wito huo aliutoa wakati akikabidhi mradi wa majengo ya huduma za afya katika kituo cha Afya Ushirombo kilichopo Kata ya Bulangwa  kwa watalamu  wa kituo hicho ili kianze kutoa  kuhuduma kwa wananchi.

Cheyo alisema iwapo watalamu wa Afya katika kituo hicho watatoa huduma vizuri kwa wagonjwa kwa kuzingatia madili itapunguza msongamano wa wagonjwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Bukombe.

"Toeni huduma bora kwa wananchi ili kupunguza msongamano katika Hospitali ya Wilaya" 


Alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Dionis Myinga kufuatilia vifaa tiba hasa vya chumba cha Upasuaji na kuhakikisha anaongeza madaktari na waunguzi wa kutosha katika kituo hicho cha afya ili kuondoa changamoto ya utoaji huduma kwa wagonjwa.


Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi kituo cha Afya Ushirombo Antony Kuya alisema Serikali ilitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wazazi, jengo la upasuaji, jengo la maabara ya kisasa, nyumba ya mtumishi, jengo la kuhifadhia maiti, jengo la kufulia nguo,  barabara ya kutembelea wagonjwa, jengo la kupokea na kusambaza umeme.


Kuya alisema mradi huo wa serikali uliletewa fedha sh 500 milioni kati ya fedha hizo zilizotumika hadi kukamilika sh 461.4 milioni na kubakiza kiasi cha sh 1.8 milioni.


Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Ushirombo Dk Henry Sahani alisema ujenzi ulianza Julai mwaka 2018 na umekamilika Februari 2019 kituo hicho cha afya ni miongoni mwa vituo nchini vilivyopata fedha toka serikali kupitia mfuko wa Afya.


Dk Sahani alisema  kabla hawajakamilisha jengo la upasuaji kulikuwa na changamoto kubwa kuanzia januari 2019 waliopewa rufaa kwenda Hospitali ya Wilaya kufanyiwa upasuaji hasa kina mama wajawazito wanaoshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.


Dk Sahani alisema kituo cha Afya Ushirombo kinapokea wagonjwa wengi  kutoka Kata jirani ya Lyambangongo, Ushirombo na Igulwa hivyo aliiomba serikali kuhakikisha inaleta vifaa vya chumba cha upasuaji na kuoongeza wataalamu wa kutosha ili kutoa huduma bora kwa wananchi.


Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe  Paul Cheyo akimkabidhi hati ya majengo  Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Kituo cha Afya Ushirombo Antony Kuya tayari kwa kuanza kutumika.


Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe  Paul Cheyo wakiwa na viongozi mbalimbali wakijiridhisha  moja ya vifaa tiba vilivyowekwa kwenye Mjengo hayo mapya




Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Dioniz Myinga akizungumza wa watumishi katika makabidhiano hayo.


Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe  Paul Cheyo wakiwa na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya majengo hayo.
 





Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa