• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Viongozi na wataalamu wapatiwa mafunzo ya ujumuishwaji wa masuala ya lishe

Imewekwa: November 18th, 2018

Viongozi na Wataalamu kutoka ngazi ya Halmashauri  ya Wilaya ya Bukombe wamepatiwa mafunzo ya ujumuishwaji wa masuala ya lishe katika mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri tarehe 16 November, 2018. Lengo likiwa ni kujadiliana kwa kina na hatimaye kuhakikisha masuala yote muhimu ya lishe yanajumuishwa katika vipaumbele vya Halmashauri vitakavyotekelezwa kupitia mipango wa bajeti.

Akifungua mafunzo  hayo Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Said Nkumba alisema “Ni dhahiri kuwa lishe bora katika jamii ni kichocheo cha maendeleo katika nyanja zote (Afya, Kilimo, Elimu, Biashara na Uchumi) na pale tu ambapo athari za lishe duni zitakapodhibitiwa au kutokomezwa ndipo malengo ya maendeleo katika nyanja hizi yataweza kufikiwa kwa ufanisi”

Mhe. Nkumba aliendelea kuelezea umuhimu wa lishe bora kwa watoto hasa katika kipindi cha siku 1000 za mwanzo wa maisha yao yaani tangu mimba kutungwa mpaka anapotimiza miaka miwili. "kipindi cha siku 1000 za mwanzo ndiyo msingi thabiti  katika ukuaji wa mwili na akili pamoja na maendeleo mazuri ya ukuaji wa ubongo, uwezo mzuri wa kukabiliana na maradhi, uwezo mkubwa wa akili za utambuzi, uwezo wa kujifunza na uwezo  wa kujiingizia kipato wakiwa watu wazima".

Naye Katibu wa afya Ndg. Remigius A. Mayasa kwa niaba ya Afisa Lishe Wilaya alisema lishe duni kwa wanawake wajawazito inawaweka katika mazingira hatarishi zaidi yanayoweza kusababisha kujifungua watoto njiti au wafu, watoto wenye mtindio wa ubongo au hata mimba kuharibika. Lishe duni huwadhoofisha wanawake wajawazito na hivyo wengi wao huugua mara kwa mara na kupata upungufu wa damu ambao huwaongezea uwezekano wa kupoteza maisha yao wenyewe na watoto wao kabla, wakati au baada ya kijififungua .

Ndg. Mayasa aliendelea kusema kuwa  hata hivyo kitengo cha lishe kinaendelea kutekeleza huduma za lishe kwa kuhakikisha kinafanya kazi ya kuelimisha jamii juu ya ulaji unaofaa kwa wanawake wajawazito, wanaonyonyesha  na  watoto wachanga  pamoja na kuboresha ulaji wa vitamini muhimu na kuzuia magonjwa yanayotokana na upungufu wa viini lishe. Aliyasema hayo wakati wa mapitio ya shughuli za lishe kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Kwa upande wake mwakilishi wa maswala ya lishe kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ndg. Peter Kaswahili alisema swala la lishe siyo la idara ya Afya pekee  yake hivyo amewataka wakuu wa idara na vitengo kuhakikisha  wanaweka shughuli za lishe katika uwaandaaji wa  bajeti  kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kwani itasaidia kuwekeza katika siku 1000 za mwanzo ambapo akili za watoto  zinaumbwa.

Akihitimisha mafunzo hayo Mkuu wa idara ya kilimo Ndg Joseph Machibya kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji  ameishukuru Serikali kupitia OR–TAMISEMI na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kuendelea kuandaa na kuendesha mafunzo  kwa wahusika katika ngazi ya Halmashauri kuhusu ujumuishwaji wa masuala lishe.


Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa