• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi wa Isemabuna wakabidhiwa vyumba 2 vya madarasa na ofisi 1

Imewekwa: November 10th, 2018

Wananchi wa kijiji cha Isemabuna kata ya Butinzya wamekabidhiwa vyumba  viwili vya madarasa, ofisi moja ya walimu pamoja na madawati 60 ya shule ya msingi Isemabuna. Msaada huo umetolewa na Ndg. Mohamed Ayobu kutoka Jumuiya ya Istiqaama Internationa iliyopo nchini Oman lengo likiwa  ni kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora itakayowasaidia kuondokana na adui ujinga.

Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Said Nkumba, viongozi wa serikali, viongozi wa dini, wanasiasa, wataalamu, walimu, wazazi pamoja na wanafunzi tarehe 10 Novemba, 2018.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Ndg. Steven S. Igoko amemshukuru Ndg. Mohamed kwa kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha miundombinu  inajengwa na ameahidi kuitunza.“Tunashukuru kwa msaada wako wa moyo wa huruma na wakujitolea. Uongozi wa shule unapenda kukuthibitishia kuwa miundombinu hiyo itatunzwa kwa nguvu  zote ili iweze kutumika kwa mda mrefu”

Aidha Mwl Igoko aliendelea kusema kuwa shule ya Isemabuna inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu pamoja na nyumba za walimu kwani mpaka sasa shule ina upungufu wa walimu 6 na nyumba 14 za walimu. Upatikanaji wa walimu pamoja na nyumba za watumishi utasaidia kufanikisha mabadiliko ya kitaaluma katika eneo la ufundishaji.

Naye Msemaji wa Jumuiya ya Istiqaama Intenational kutoka kanda ya Ziwa Ndg. Juma Ismail alisema jumuiya hiyo imeishaonyesha mwanga katika Wilaya ya Bukombe pia inafanya kazi katika nchi ya Ghana, Nigeria, Kenya, Mali na Afrika ya Kusini ili kuwasogezea huduma bora wananchi wote pasipo kuangalia itikadi zao za kidini.

Akiongea katika  Makabidhiano hayo Ndg. Mohamed Ayobu ameahidi kujenga Msikiti na kutoa Tsh 5,000,000.00 kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa Zahanati ambayo ni sadaka yake kwa wananchi wa kijiji hicho ili kusogeza huduma kwa akina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano. Pia amewashukuru wananchi kwa kuacha shughuli zao na kuhudhuria sherehe za makabidhiano hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Nkumba ameishukuru Jumuia ya Istiqaama International kutoka Oman kwa niaba ya Serikali kwa kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi.”Natoa shukrani zangu kwa niaba ya serikali kwani kutoa ni moyo na ni njia mojawapo ya kujiwekea hazina kwa Mwenyezi Mungu, Kwani mmetumia nguvu zenu kwa ajiri ya kutatua matatizo ya wananchi”

Pia Mhe. Nkumba ametoa tahadhari kwa wazazi wasiotaka watoto wa kike wasiendelee na masomo ya Sekondari.”Sitapenda kuona  watoto wa kike waliomaliza shule za msingi na kufaulu kwenda sekondari wanaozeshwa   na kama mmekwishapokea mahali  kwa watoto waliofaulu kwenda sekondari kakikisheni mnarudisha fedha kwani ninawahakikishia kuwa harusi  hizo hazitafanyika”

DC Nkumba amewagiza viongozi wa makanisa na misikiti kuhakikisha wanajiridhisha na ndoa zinazofungwa.”Masheikh, Wachungaji na Maparoko kama mnafungisha ndoa hakikisheni mnajiridhisha na ndoa hizo kama ni wanafunzi ama si wanafunzi vinginevyo tutawakamata na kuwaweka ndani na kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake, tunataka mabinti zetu wasome”

Jumuiya ya Istiqaama International imeweza kukarabati vyumba 4 vya madarasa pamoja na visima viwili vya maji. kwa historia shule ya Msingi Isemabuna ilianzishwa mwaka 2002 mpaka sasa ina jumla ya wanafunzi 616 kuanzia darasa la awali hadi darasa la saba wavulana wakiwa 331 na wasichana 285 na jumla ya walimu 8.


Ndg.Mohamed Ayobu akiongea na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Isemabuna.

Baadhi ya madawati yaliyotolewa na Jumuia ya Istiqaama Internatinal.


Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Ndg Said Nkumba akitoa shukrani kwa niaba ya Serikali kwa Jumuia ya Istiqaama International.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa