• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DC Nkumba Nkumba Awapongeza Walimu Ufaulu Kidato cha Nne.

Imewekwa: January 28th, 2022


Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Said Nkumba amewapongeza walimu pamoja na wadau wa elimu kwa kuwezesha wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao ya kuhitimu kidato cha nne.

"Ninawapongeza walimu, wamefanya kazi kubwa ya kuhakikisha watoto wetu wanafaulu. Kimkoa tumekuwa wa kwanza matokeo ya kidato cha nne na cha pili vile vile matokeo ya darasa la sana tumeshika nafasi ya pili kimkoa."

"Mimi pamoja na watumishi wenzangu wa serikali tupo imara kwa ajili ya kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika sekta zote."

Pongezi hizo amezitoa leo tarehe 28 Januari, 2023 wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Bukombe.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2020 - 2025 kwa kipindi cha Julai - Disemba 2021 Nkumba amesema Idara ya Afya imepokea kiasi cha shilingi Milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Bufanka, Milioni 300 kwa ajili ya upanuzi wa kituo cha Afya Bulega, Milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la dharura hospitali ya Wilaya ya Bukombe na Milioni 90 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 2 za watumishi wa afya.

Aidha Idara ya Elimu Msingi imetumia kiasi cha Shilingi Milioni 789.2 kati ya 860 zilizotolewa kutokana na Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO - 19 katika ujenzi wa vyumba 43 katika shule za Msingi shikizi 10. Mnamo tarehe 25 Disemba, 2021 halmashauri ilipokea tena kiasi cha shilingi Milioni 112.5 kwa ajili ya ukamilishaji wa shule za msingi 5 fedha kutoka serikali Kuu.

Kwa upande wa Idara ya Elimu Sekondari halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi Bilioni 2.1 fedha kutoka Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO - 19 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 64 vya madarasa katika shule za sekondari 17, Milioni 150 kwa ajili ya ukamilishaji wa Maabara, Milioni 112 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari 5 na Milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari Ng'anzo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko amempongeza Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.

"Rais anamapenzi ya dhati na Wilaya ya Bukombe na Taifa kwa ujumla ndiyo maana amezidi kutoa Mamilioni ya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aidha amewataka wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama kupendana na kuwa na umoja ili kuijenga Bukombe.

"Tupendane, tuwe na umoja na tuthaminiane ili tuweze kuijenga Bukombe yetu."

Walioshiriki kikao hicho ni pamoja na wajumbe wa halmashauri Kuu ya Wilaya CCM, wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wakuu wa Taasisi za Serikali.







Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa