• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DKT. Msonde Awaagiza Wajumbe wa Timu za Usimamizi Mradi wa BOOST Kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu

Imewekwa: December 23rd, 2022

Angela Msimbira MWANZA

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde amewaagiza Wajumbe wa Timu za Usimamizi wa Utekelezaji wa Mradi wa  Uboreshaji wa miundombinu ya  Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) kuhakikisha wanafuata  sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Ametoa agizo hilo  leo tarehe 23 Disemba, 2022 wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa timu  za utekelezaji wa Mradi wa Boost  kwa Mikoa ya Mwanza, Geita na Mara yaliyofanyika  katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Butimba Jijini Mwanza. 

Dkt. Msonde ameonya vikali tabia  ya kufanya maamuzi kinyume na taratibu kwa kuwa kufanya hivyo kutafelisha utekelezaji wa afua zilizowekwa na Mradi, hivyo kuzingatia Sheria, taratibu, kanuni na miongozo kutasaidia kupunguza hoja za wakaguzi katika utekelezaji wa  mradi huo.

Amewataka wajumbe hao kutokubadilisha maeneo ya utekelezaji wa mradi  ya ujenzi wa miundombinu ya shule au mradi uliopangwa kutekelezwa bila kupata kibali kutoka  Ofisi ya Rais –TAMISEMI kwa kufanya kinyume na maagizo  kutaleta dosari kwenye  mradi.

 “ Kumekuwa na tabia ya kubadilisha maeneo ya ujenzi wa shule na miradi mingine, hilo halikubaliki katika utekelezaji wa mradi wa Boost, mradi huu ukipangiwa kufanya kazi  katika eneo fulani la ukarabati au ujenzi, hapo ndipo pajengwe kama kutahitaji mabadiliko ni lazima kupata kibali  kutoka Ofisi ya Rais - TAMISEMI” amesisitiza Dkt. Msonde

Amesema kuwa maeneo ambayo yatafanyiwa ukarabati na kujengwa yamefanyiwa tathmini na imetolewa katika vitabu, hivyo haitakiwi kubadilishwa  bila kupata kibali kutoka  Serikalini

Dkt. Msonde amewaagiza wajumbe hao kuhakikisha katika afua zote nane walizopitishwa wanaziwekea mkazo kwa kutumia nguvu, akili na utashi kwa kuhakikisha afua zote zinatekelezwa na kukamilika kwa wakati uliopangwa.

Aidha, amewataka kudumisha ushirikiano kwenye utekelezaji wa mradi wa Boost kila mmoja kwenye kada yake kwa kuhakikisha wote wanaongea lugha nmoja ili ufanisi wa mradi huo uweze kutokea.

Naye Afisa Elimu  Mkoa Mara   Benjamin Oganga ameishukuru Serikali kwa kuamua kutoa Mafunzo ya kuwajengea uwezo timu za Usimamizi za Utekelezaji wa Mradi wa Boost nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa weledi na kutoa matokeo chanya kwa jamii.



Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa