• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Gharama za Kuunganisha Huduma ya Maji Ziwe Rafiki

Imewekwa: January 17th, 2023

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mhe.Yusuph Mohamed Yusuph mmoja wa wajumbe wa kamati ya Siasa Wilaya amemtaka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Ushirombo kuhakikisha bei ya kuunganishwa na huduma ya maji inakuwa rafiki ili wakazi wa mji wa Ushirombo waweze kunufaika na mradi wa Uboreshaji wa Huduma ya Maji katika Mji wa Ushirombo.

"Ni matamanio yangu kuona wakazi wote wa mji wa Ushirombo wanaunganishwa na huduma ya maji safi na salama kwa gharama nafuu kupitia mradi wa uboreshaji wa huduma za maji katika mji wa Ushirombo."

Yusuph ameyasema hayo tarehe 16 Januari, 2023 wakati wa ziara ya kamati ya siasa Wilaya ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo  Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji Ushirombo  Getruda Deogratius alisema mradi wa Uboreshaji wa Huduma ya Maji katika mji wa Ushirombo unatarajia kuhudumia wakazi wapatao 29,672. Chanzo cha maji katika mradi huo ni visima viwili virefu vyenye uwezo wa kuzalisha maji jumla ya lita 19,700 kwa saa na hadi sasa mradi huu umakamilika kwa asilimia 95. 

Aidha aliendelea kusema kuwa  mradi huo utakapokamilika utapunguza muda wa kufuata maji umbali mrefu ambapo  muda huo utatumika kufanya shughuli nyingine za kiuchumi pamoja na kupunguza uwepo wa magonjwa yanayotokana na matumizi ya  maji yasiyo safi na salama kama vile kuhara, homa ya matumbo na kipindupindu.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Wilaya Matondo Lutonja  ameupongeza uongozi wa Mamlaka kwa usimamuzi mzuri wa mradi huo, vile vile ameshauri kuwa matangazo yatolewe ili wananchi waweze kufahamu uwepo wa huduma ya maji safi na salama na kisha kuunganishiwa.

Mradi wa Uboreshaji wa huduma ya maji katika mji wa Ushirombo unatekelezwa kwa mikataba mitatu (Mkandarasi wa ujenzi, Mzabuni wa pampu na mzabuni wa bomba) kwa gharama ya shilingi 859,395,343.85 chini ya program ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko - 19 pamoja na Malipo kulingana na Matokeo (EP4R).


Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa