• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

“Haya Mema tulioanza leo yaendelezwe katika Wilaya ya Bukombe”

Imewekwa: May 3rd, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi ameshiriki ujenzi wa Zahanati katika Vijiji Vya Nampalahala, Kabagole, Nakayenze kata ya Busonzo na Kijiji cha Shilabela kilichopo kata ya Namonge Wilaya ya Bukombe hivi leo.

Katika Ziara hiyo Mkuu wa Mkoa amewasihi Wananchi Kufanya kazi ili kujiletea Maendeleo”Hakuna Maendeleo yanayoletwa bila kufanya kazi” alisema Luhumbi

Mkuu wa mkoa amefafanua Wilaya ya Bukombe ina jumla ya Vijiji 52, mpaka sasa vijiji 27 bado ujenzi wa Zahanati havijaanza, kwakuwa ujenzi huu ni endelevu mpaka kufikia mwezi julai hatua mbalimbali za ujenzi zitakuwa zimefikiwa, pia amewataka Wananchi wa wilaya ya Bukombe, wanaojihusisha na mauhusiano ya kimapenzi na wanafunzi wa kike kuacha mara moja, kwani kesi za mimba katika mkoa wa Geita ambapo pia wilaya ya Bukombe ipo zimekuwa nyingi, hivyo kupelekea watoto wa kike kukatisha ndoto zao, huku wahusika wakiendelea kuvuruga watoto wa kike wengine  mitaani, “kwa wanaowavuruga watoto wa kike kwa sasa mkoa wa Geita Sio Sehemu ya kuishi, mimba haikubaliki Geita ” alisema Luhumbi

Katika kuhakikisha dhamira ya kutokomeza Mimba kwa watoto wa kike zinakwisha kabisa, kila kijiji ambacho ameshiriki ujenzi wa Zahanati Mkuu wa Mkoa ametoa namba zake za Simu kwa Wananchi ili kupokea kero zao, maoni yao na kupokea za Mimba kwa watoto wa kike moja kwa moja, na amepiga marufuku kukaa na taarifa za mimba zaidi ya masaa 48.

Aidha Mkuu wa Mkoa amesisitiza Wananchi wapewe semina ya uanzishaji wa Vikundi vya Vijana na wakina Mama ili wapate Mikopo, amemuagiza Afisa Maendeleo ya wilaya kuhakikisha anatembelea vijiji vyote 52 kutoa semina ya namna ya kutengeneza vikundi vyenye tija.

Wananchi wakiweka zege kwenye Msingi wa Zahanati ya Nampalahala ili Mkuu wa Mkoa wa Geita(Mwenye Nguo nyeupe) aweze kusawazisha zege hilo.

Msingi wa Zahanati ya Nampalahala uliochimbwa leo.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi akichanganya mchanga na Cementi akishirikiana na Wananchi.


Diwani wa Kata ya Busonzo Mhe.Safari Nicas Mayala akiongea na Wananchi wa kata yake “Mkuu wa Mkoa ameleta chachu ya Maendeleo kwa wana Bukombe tumuonyeshe tunaweza, hakuna Mkuu wa Mkoa aliyewahi kufanya hamasa hii katika Mkoa wetu, tumuunge mkono”.

Wananchi wakisikiliza ujumbe wa Maendeleo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi akimalizia kusawazisha Msingi wa Zahanati ya Kabagole.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Josephat Maganga akisawazisha Msingi wa Ujenzi wa Zahanati kijiji cha Kabagole.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi akiongea na Wananchi “ Haya Mema tuliyoanza leo yaendelezwe, ujenzi wa Nguvu wa Zahanati.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Josephat Maganga kupanga Mawe kwenye Msingi wa Zahanati Kijiji cha Shilabela kata ya Namonge.

Wakina Mama waliojitokeza na kusomba maji ya Ujenzi wa Zahanati kijiji cha Shilabela Kata ya Namonge.

Wakina Mama waliojitokeza na kusomba maji ya Ujenzi wa Zahanati kijiji cha Shilabela Kata ya Namonge.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ambaye pia ni Diwani wa kata ya Busonzo Mhe.Safari Nicas Mayala(Mwenye kofia Nyeupe shati la kijani , ameshikilia ndoo ya njano akimwanga zege) huku Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Robert Gabriel ambaye ni Mhandisi wa masuala ya ujenzi akisawazisha zege

Wananchi waliojitokeza kushiriki ujenzi huo kijiji cha Shilabela

Msingi wa Ujenzi wa Zahanati kijiji cha Shilabela Kata ya Namonge

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC MURAGILI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE ROBO YA TATU (Januari-Machi 2024/2025)

    May 08, 2025
  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkutano wa baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya 3 kwa mwaka 2024/2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa