• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wanawake kuanzisha Kiwanda cha uchakataji mihogo Wilaya ya Bukombe

Imewekwa: March 8th, 2018

Mkuu wa mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel ametoa hati ya uzinduzi kwa kikundi cha Saccos ya kina mama,na kuendesha harambee  ndogo ya kuanzisha kiwanda cha uchakataji Mihogo kwa Jukwaa la Wanawake Kiuchumi,ambapo amechangia kiasi cha Tsh.500,000/= na kuungwa mkono  na Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Naibu Waziri wa Madini mhe.Dotto Biteko ambaye pia amechangia Tsh.500,000/=,pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na vyama vya siasa katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika wilayani Bukombe.

Katika Maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa amewaagiza wakurugenzi wote  wa Halmashauri za mkoa  wa Geita kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili  ya vikundi  vya wanawake(4%), vijana(4%) na watu wenye ulemavu (2%) ili wajikwamue kiuchumi kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali  ili kuongeza kipato.

Mhandisi Robert Gabriel amesema serikali ya awamu ya tano  ina lenga kuhakikisha Tanzania inakua nchi ya uchumi wa viwanda  “Wanawake wanamchango mkubwa katika  harakati za kuchochea ukuaji  wa uchumi ndani ya nchi  kupitia vikundi vya kiuchumi kama VICOBA na shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile  uchakataji wa malighafi  na kuongeza thamani ,ufugaji; kilimo cha bustani na matunda” amesema Mhandisi Robert

Maneno haya ya Mkuu wa Mkoa yanaenda sambamba kabisa na kauli mbiu ya mwaka huu inayosema Kuelekea Uchumi wa Viwanda “Tuimarishe usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake vijijini.

Pia amezitaka  halmashauri kutambua  vikundi vya wanawake  na vijana  vyenye mwelekeo  wa viwanda  na kukuzalisha  malighafi kwa  ajili ya kulisha viwanda  vidogo  na vya kati ili vijengwe  uwezo kifedha , mafunzo na vifaa ili vichangie azma ya serikali.

Mkuu wa mkoa ametoa wito kwa jamii kuwalinda wanawake,wasichana dhidi ya vitendo vya ukatili  kimwili kama  vipigo, ubakaji, ndoa za utotoni na kuwarubuni kimapenzi hivyo kupelekea kukatisha ndoto zao za kujiendeleza kiuchumi, na kurudisha  nyuma maendeleo ya kiuchumi  katika ngazi ya kaya  na taifa.

Mwenyekiti wa Saccos Iliyozinduliwa Na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akipokea Hati ya Uzinduzi wa Saccos Hiyo.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilayani Bukombe Bi.Leticia Akisoma Risala Wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Akitembelea wajasiliamali Wanawake Katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe.Dotto Biteko akitoa Tsh .500,000/= Katika Harambee ya Uanzishaji wa Kiwanda cha Uchakataji Mihogo Kwa Jukwaa la Wanawake Bukombe.

Mkuu wa Mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel akimlisha Kipande Cha Keki Mwenyekiti wa Chama CCM Wilaya ya Mbogwe Bi Johari Juma Baada ya Kuchangia Harambee ya Uanzishaji wa Kiwanda cha Uchakataji Mihogo.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Josephata Maganga akichangia Harambee Ndogo ya Kuchangia Uanzishwaji wa Kiwanda cha Uchakataji Mihogo.

Maandamano ya Wanawake katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Leo Machi 8,2018 Wilayani Bukombe.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa