• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kikundi cha MAGUKO chazinduliwa rasmi

Imewekwa: January 2nd, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Said J. Nkumba leo tarehe 2 Januari, 2019 amezindua rasmi kikundi cha Maisha yangu ni maisha yako (MAGUKO) chenye madhumuni ya kusaidiana na Serikali pamoja na wananchi katika kuchangia, kukusanya na kuhakikisha uwepo wa damu ya kutosha wakati wote katika benki ya damu salama kupitia mpango maalumu wa “Tumia Damu Rudisha Damu.”

Mhe. Nkumba amewapongeza na kuwatakia kila la heri wanakikundi wa MAGUKO katika kazi  ya uzalendo wanayoenda kuifanya ya kuhakikisha benki ya damu katika Hospitali ya Wilaya ya Bukombe inapata damu ya kutosha ambayo itaweza kuwasaidia wananchi wote pindi wanapopata matatizo ya upungufu wa damu.

Aidha Mhe. Nkumba amewahakikishia wanachama wa MAGUKO kuwa changamoto zote walizoziwasilisha, ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji itazipitia na kuzifanyia kazi na amewapatia kiasi cha Tsh 100,000.00 (Laki moja) ikiwa ni kuwaunga mkono kwa ajili ya kutunisha mfuko wa kikundi ili waweze kusonga mbele. Pia amemuomba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  ya Wilaya ya Bukombe kuhakikisha anatoa taarifa ya kikundi hicho kwenye vikao vya Waheshimiwa Madiwani ili waweze kuwahamasisha wananchi kuchangia damu pindi wanapokuwa kwenye mikutano ya hadhara.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Ndg Dionis Myinga amewapongeza wanakikundi kwa jitihada wanazozifanya za kuhakikisha damu safi na salama inapatikana katika hospitali ya Wilaya kwa kufanya hivyo wataweza kuokoa maisha ya akinamama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe inamahitaji ya chupa za damu 2584 kwa mwaka, chumba 216 kwa mwezi na chupa 8 kwa kila siku kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa ambao wanakadiliwa kuwa na uhitaji wa kuongezewa damu kutokana na sababu mbalimbali. Hayo ameyasema Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya ya Bukombe Dr. Range Nyamhanga wakati akitoa taarifa ya damu salama.

Naye Katibu Msaidizi wa kikundi cha MAGUKO Ndg Macrina Bileha amesema changamoto wanazokabiliananazo ni pamoja na ukosefu wa usafiri, ukosefu wa vifaa vya hamasa na burudani (muziki) na ukosefu wa elimu ya zoezi hilo.

Kwa upande wake mwanakikundi wa MAGUKO Ndg. Frolah Bernad ametoa wito kwa jamii kuhakikisha inawapokea vizuri. “ Tunaomba wananchi watupokea  pindi tunapoenda kuhamasisha uchangiaji wa damu salama na tutambue kuwa jukumu la uchangiaji wa damu ni jukumu la wananchi wote hivyo  tushirikiane kwa pamoja na hatimaye tuwe na akiba ya kutosha katika benki ya damu.”

Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ina jumla ya vituo viwili vyenye uwezo wa kutoa huduma ya damu kwa wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu salama ambavyo ni Hospitali ya Wilaya ya Bukombe pamoja na kituo cha afya Uyovu.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC MURAGILI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE ROBO YA TATU (Januari-Machi 2024/2025)

    May 08, 2025
  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkutano wa baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya 3 kwa mwaka 2024/2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa