• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Madiwani kutatua changamoto ya usafiri

Imewekwa: September 9th, 2022

Madiwani wilayani Bukombe waiondolea uvivu kero  ya uhaba wa vyombo vya usafiri  kwa niaba ya wananchi katika kikao cha Baraza la madiwani hapo jana licha ya kuwa viongozi mbalimbali walishikamana na kufanikisha kupunguza adha hii kwa namna Fulani ndani ya miaka mitano iliyo pita.

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa kikao cha waheshimiwa Madiwani hapo jana Diwani kata ya BusonzoMh. Mlalu Bundala Maziku aliibua hoja kuu ambayo imekuwa ikitolewa na wananchi wengi nayo ni juu ya Uhaba wavyombo vya usafiri unaosababishwa na kuzuiwa hivi karibuni kwa magari aina ya(Pro box) mchomoko kutumika kwa ajili ya kusafirisha abiria huku akieleza kuwa kwanini baadhi ya maeneo bado zinatumika.

  “Mh.Mwenyekiti kuna jambo ambalo limekuwa ni adha kubwa hususani katika mji wa Ushirombo na Runzewe juu ya Usafirishaji wa abiria kwa kutumia magari aina ya Pro-Box ambayo yamezuiliwa kufanya shughuli zake za usafirishaji wa abiria jambo ambalo limekuwa ni kero na changamoto lakini nadhani ni maelekezo yaviongozi licha ya kuwa maeneo kama Kagera na Biharamulo yanaendelea kufanya kazi kama kawaida”Mh.Mlalu alieleza

Aidha naye Diwani wa kata ya Busonzo Mh.Safari Nicas Mayala alimpongeza Mh.Diwani wa kata ya Namonge kwa hoja adhimu aliyo iibua huku akieleza kuwa wao kama wawakilishi wa wananchi na kukazia kuwa kutotumika kwa aina ya magari hayo kumeleta adha kubwa sana huku akisema hata yeye amekuwa ni mhangwa wa janga hilo na kumpelekea kutumia Roli kama nyezo ya usafiri kwa majuma kadhaa yaliyo pita huku akihitaji majibu ya hoja hiyo.

“Mh.Mwenyekiti sisi ni wawakilishiwa wananchi tunao wajibu wa kutetea maslahi ya wananchi mbalimbali wajasiriamali na watu wa aina zote suala la magari haya aina ya Pro-box kutotumika kama nyenzo ya kurahisisha usafiri wa abiria yameleta  adha  kubwa sana mimi nilizungumze kwa sababu nimekuwa mhanga wa tatizo hili kwani juzi nilikosa usafiri na nikalazimika kutumia usafiri wa roli ningeomba majibu katika hili.Diwani kata ya Busonzo aliongezea

Hata hivyo aliendelea kusisitiza kuwa katika dira ya Chama cha mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025 kwenye mpango kazi wa MKUKUTA inaelezea kuwa kutakuwepo na utaratibu maalumu wa kuzitambua na kuimarisha sekta binafsi huku sera hiyo ikieleza ni kwa namna gani wananchi wataweza kubuni namna ya kujipatia kipato na kusema kuwa hata magari hayo yaliyo zuiliwa kufanya shughuli za usafirishaji wa abiria ni ya wajasiriamali ambao walichukua mikopo na kwa kipidi hicho yalisajiliwa na kufanya kazi.

Naye kwa upande wake kamanda wa polisi wilaya ya Bukombe Afisa Mokiri Mkenye baada ya kutupiwa lawama na Waheshimiwa madiwani juu ya kero iliyojitokeza alieleza kuwa hoja hii ni ya kisheria ambayo inaeleza gari ndogo hazina mamlaka ya kusafirisha abiria kwa mujibu wa sheria za LATRA na kutolea ufafanuzi kuwa gari hizo zinatakiwa kutumika punde tu zitakapo kodiwa.

“Nipende kuliweka sawa jambo hili kwani lawama nyingi zimeelekezwa kwenye vyombo vya usalama kwani tukilejelea katika sheria ya LATRA inaeleza kuwa gari hizo ndogo aina ya Pro- box haziruhusiwi kubeba abiria ila tu zinatumika endapo kama zimekodiwa kwa ajiri ya kurahisisha shughuli za usafiri na hivyo ndivyo ilivyo na hapo awali zilitumika kimakosa “OCS wilaya ya Bukombealitolea ufafanuzi katika hilo

Vilevile, Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe Leokadia Kasase naye alianza kwa kuwashukuru wauliza maswali na kusikitika kutokana na majibu ya Kamanda wa polisi wilaya huku akieleza kuwa mkoa wa Geita una wilaya 5 ambapo gari hizo zinatumika kubebea abiria katika wilaya nyingine isipokuwa Bukombe na kutoa rai kwa waheshimiwa madiwani kuungana kwa pamoja kutetea maslahi ya wanabukombe kwa ujumla.

“ Nianze kwa kusikita kwa majibu ya kamanda wa polisi wilaya na sijajua kama ufafanuzi alio utoa upo sahihi maana kutoka Gita kwenda Rwenzera gari hizo zinafanya kazi ,Mkoa wa Kagera ,Biharamlo kuelekea Nyakanazi ,Kibondo,Kakonko kama kweli vyomo vya usalama vinasimamia sheria na inatumikanchi nzima kwanini wilaya ya Bukombe tu ndiyo hazitumiki nipende kuwaomba viongozi wenzangu tushirikiane kutetea maslahi ya wananchi wetu” Mh.Makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Bukombe alizungumza

Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Mh.Daniel Machongo alieleza kuwa suala hili limeshika hatamu na kuwa ni miongoni mwa adha kubwa kwa wananchi na hata vingozi kwa ujumla na kueleza kuwa mnamo mwaka 2017 kero hii ilijitokeza na kufanyiwa ufumbuzi kwa kushirikiana na hayati rais John Pombe Magufuli.

“Adha hii ya ufinyu wa vyombo vya usafiri limekuwa ni gumzo kwa waheshimiwa viongozi na kwa wananchi pia kwa lilishawahi kutokea kwa kipindi cha miaka mitano iliyo pita kwa ushirikiano wa Naibu waziri wa mambo ya ndani kwa wakati huo Mh.Dotto Biteko na rais wajamhuri ya muungano wa Tanzania kwa wakati huo na likawa limekwisha “Alieleza Mwenyekiti chama cha mapinduzi wilaya ya Bukombe

Aidha Mh.Daniel Machongo alimalizia kwa kusema kuwa magari hayo madogo ni nyenzo ya usafiri pia kwa namna nyingine ni sehemu ya ajira kwa wananchi ambao walikuwa ni waongozaji wa vyombo hivyo na wamiliki wake pia na kuviomba vyombo vya usalama na ngazi za juu za serikali kuliwekea mkazo na utatuzi katika kero hiyo.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa