• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Maonesho ya nne ya Madini yaifurahisha kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.

Imewekwa: September 16th, 2021

Leo Septemba 16, 2021 maonesho ya Nne ya Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yameanza kwenye Viwanja vya maonesho Bombambili Mjini Geita na kwa baraka kubwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Nishati na madini wametembelea maonesho hayo.

Wabunge wa Kamati hiyo walioongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati wamesema wamefurahishwa sana na namna Waandaaji walivyozingatia Washiriki kutoka sekta za Madini katika kuhakikisha Elimu ya teknolojia katika sekta ya madini inawafikia wachimbaji wakubwa na wadogo kwa kupata elimu ya teknolojia mpya ya uchimbaji.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Mheshimiwa Seif Gulamali amesema kuwa shughuli za uchimbaji wa madini zinahusisha teknolojia za aina mbalimbali hivyo maonyesho hayo yatasaidia watu wengi hasa wachimbaji kutoka Kanda ya ziwa kujifunza teknolojia mpya ya uchimbaji.

Mhe. Gulamali amefafanua kuwa shughuli za uchimbaji unaohusisha matumizi ya Zebaki yanachangia kwa kiwango kikubwa kusababisha ugonjwa wa Saratani na kwamba taarifa nyingi zinaonesha kuwa wagonjwa wengi wa saratani wanapatikana katika mikoa ya Kanda ya ziwa hivyo husafiri kwenda kutibiwa jijini Dar es salaam katika Hospitali ya Ocean road ni mzigo mkubwa kwa wagonjwa.

Aidha, ameshauri serikali pamoja na wadau wa maendeleo Kama mgodi wa kuchimba Dhahabu wa Geita (GGML) kujenga Hospitali ya kutibu Saratani katika Kanda ya ziwa ili kupambana na ugonjwa huo au kuongeza nguvu kwenye juhudi zilizoanzishwa na Hospitali ya Kanda ya Bugando ambao wameshaanza juhudi za kujenga na kupata vifaa kwa ajili ya matibabu ya Ugonjwa huo.

Mwenyekiti Seif Gulamali amesema taasisi za Wizara ya Madini Kama Shirika la madini la taifa (Stamico), Taasisi ya utafiti na jiolojia Tanzania ( GST) na taasisi ya uhamasishaji uwazi katika sekta ya uzinduaji ( Teiti) zinaendelea kutoa huduma katika maonyesho hayo kwa wachimbaji wa madini.

Naibu waziri wa Madini Profesa Shukrani Manya amesema lengo kuu la kuanzishwa kwa maonyesho  hayo ni kukutanisha pamoja wachimbaji wakubwa na wadogo na wadau mbalimbali katika sekta ya madini ili kubadilishana teknolojia huku akifafanua kuwa katika sekta ya uchimbaji Kuna Mambo mengi ya kujifunza ambayo yanabadilika kila siku.

Mkuu wa mkoa wa Geita, Mhe. Rosemary Senyamule amesema kuwa watu watakao tembelea mabanda ya maonyesho watanufaika na kupata elimu kuhusu sekta ya madini pamoja na kukutana na wadau wengine katika sekta hiyo, kupata fursa za biashara na kujifunza teknolojia mbalimbali za kuchimba madini.

Aidha, Mhe. Senyamule ametoa wito kwa wachimbaji wadogo kushiriki maonesho hayo ambayo yamewalenga zaidi na kwamba maonyesho hayo yatatukika kuwapa elimu kuhusu matumizi ya teknolojia mpya isiyotumia Zebaki kwenye uzalishaji wa dhahabu.

Mkuu wa mkoa Senyamule ameongeza kuwa katika maonyesho hayo tahadhari zote za kujikinga na uviko19 zimezingatiwa kama kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono,na kuvaa Barakoa.

Meneja wa Mashiriko kutoka Mgodi wa kuchimba madini ya dhahabu wa Geita (GGML), Ndugu, Manace Ndoroma amesema kuwa mgodi huo unatumia maonyesho hayo kuonyesha teknolojia mpya ya uchimbaji na kwamba kwenye maonyesho hayo GGML itatoa mafunzo namna wanavyotoa huduma za afya hasa wafanyakazi wanapopata ajali katika shughuli za uchimbaji.

Paul Zahoro

Geita RS.







Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa