• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mchango wa sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa waongezeka.

Imewekwa: September 27th, 2021

Waziri wa Fedha na mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema mchango wa sekta ya Madini kwenye pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 3 mwaka 2018 hadi 6 mwaka huu na kwamba pamoja na mambo mengine mchango huo umechangiwa na maboresho ya sera na sheria za Madini yaliyofanyika ili kuhakikisha Sekta hiyo inaendelea kukua.

Waziri Nchemba amesema hayo leo Septemba 26, 2021 wakati wa hafla ya kilele cha maonesho ya Madini 2021 yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZA-Bombambili mjini Geita ambapo alikua mgeni rasmi wa hafla hiyo kwa niaba ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Mpango.

Mhe. Nchemba amesema serikali kupitia Benki ya Kuu (BoT) imejipanga kununua madini safi kutoka kwenye viwanda vya kusafisha dhahabu kuyahifadhi na kuyaongezea thamani ili kufikia lengo la kuongeza mchango wa sekta ya madini kwenye pato la Taifa hadi kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.

“Sasa muda umefika kwa watanzania kuanza kutengeneza viwanda vya kuchakata madini yetu na kiupekee nimpongeze mama jasiri Sarah Masasi kwa kujenga kiwanda chenye teknolojia ya kuchakata dhahabu kwa asilimia ya 99.9 kwa kufanya hivyo tutauza dhahabu yetu ikiwa na ubora wa hali ya juu na hivyo pato la Taifa litakua” amesema Mhe. Nchemba.

Hata hivyo, amezipongeza taasisi zote zilizotoa Elimu kwa wadau na wananchi waliotembelea maonesho ya Nne ya Madini Geita na amewataka wote walionufaika na maonesho hayo kwenda kuifikisha Elimu hiyo kwa wengine ili kusaidia Sekta nzima.

“Serikali tayari imeshafanya kazi yake ya kubadilisha sheria ambayo imelenga kuwanufaisha watu wote ikiwemo Serikali yenyewe wawekezaji na wananchi kwa ujumla kupitia mfuko wa huduma za jamii kazi kubwa iliyopo kwa watendaji na wananchi kwa ujumla kuona kuwa ni jukumu lao kuilinda miradi inayojengwa kupitia fedha za CSR na fedha zinazotoka Serikalini, huu ni wajibu wa kila mtu kwani hiyo ni mali yao kwa faida zao na jamii kwa ujumla” Mhe. Nchemba ameeleza.

"Mhe. Rais amejidhatiti anakwenda kujenga madarasa zaidi ya elfu kumi na moja nchi nzima, niwaombe tu viongozi wote tusaidiane kwenye Usimamizi wa shughuli hizi na hakuna kitu mama anakifuatilia kama fedha hizi na sisi wasaidizi wake tunakwenda kumsaidia kwenye hilo."

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Rosemary Senyamule amempongeza Mhe. Dkt Nchemba kwa Usimamizi mzuri na wizara na kuongoza kwenye ukusasanyaji wa mapato ya serikali kwa kipindi cha hivi karibuni.

"Nikupongeze sana Mhe. Waziri kwa kazi nzuri unayofanya na kuaminiwa na Mhe. Rais na kuwa mtunza kihenge cha Serikali."

"Maonesho ya 2021 yameongeza mvuto na umahiri, tumesikia awali kwenye taarifa kuwa Washiriki wa maonesho yaliyopita walikua 338 mwaka jana na mwaka huu waongezeka na kufika 498 huku wananchi waliozungukia mabanda ni wastani wa watu elfu 10 hadi 12 kwa siku, na maonesho yetu yamekua na sura ya kimataifa." Mhe. Mkuu wa Mkoa.

Wakati huohuo, Mhe. Mkuu wa Mkoa amewataka wafanyabiashara wa wadau wa dhabau kuiongezea dhamani ili kufanya iwe Bora na kuleta tija zaidi. "Moja ya mazao katika Mkoa wetu wa Geita ni Dhahabu, Mhe. Mgeni rasmi kama ulivyoona Kiwanda Cha kuongeza dhamani kwenye Madini, tunataka mtu akija Geita akutane na mtaa wa Dhahabu",amesema.

Vilevile, Mhe. Mkuu wa Mkoaamesema Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ametoa bilioni 4.5 kwa ajili ya Kujenga Stendi ya kisasa ya mabasi Mkoani Geita na kwamba uwepo wa Stendi hiyo utasaidia kuondosha shughuli hizo kutoka kwenye Stendi yenye matope.

Mhe. Mkuu wa Mkoa ametumia wasaa huo kuwakaribisha wananchi kwenye Sherehe za kilele cha mwenge wa Uhuru zitakazofanyika Oktoba 14, 2021 Wilayani Chato ambapo Mgeni rasmi atakua Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 “Sisi kama wizara tuendelea kuimarisha mifumo ya kudhibiti utoroshaji wa madini kwani mpaka sasa bado wapo wachache ambao bado wanatorosha madini yetu na tunaandaa sheria kali ya kuwakamata wale wote wanaovusha madini kwa njia ya panya kwani wanapoteza mapato ya Serikali” Mhe. Profesa Manya.

“GGM inaona fahari kuwa chachu ya maendeleo kwa Mkoa wa Geita na kuwa kinara wa uchangiaji wa kodi na uchangiaji wa maendeleo ya jamii na tunaahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa Mkoa wa Geita”, amesema Makamu wa Rais wa Mgodi wa Dhahabu Geita, Saimon Shayo.

"WanaGeita nawapongeza kwa mwaka huu kuwa na Mapato makubwa mkiongozwa na Nyang'hwale, hongereni sana pia niwaombe Wizara ya Madini waanzishe masomo kwa kushirikiana na VETA ili wataalamu wa kuchimba watokee kule." amesema Kanali Lubinga.

Alhaji Kalidushi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita ametoa wito kwa taasisi za kifedha na mabenki kutoa Mikopo kwa wachimbaji yenye masharti nafuu ili iwasaidie kuwainua kutoka Uchimbaji mdogo kwenda juu.

"Wapo wachimbaji wana leseni sasa ukiwawezesha itasaidia kuwainua kiuchumi," amesema.

"Ndani ya miezi Sita ya Uongozi wa Rais Samia Kanda ya ziwa imepata Miradi mingi na mikubwa aidha ya kuendelezwa pamoja  na Meli mpya zimeendelea kujengwaa kama ile kubwa ya mizigo kwa zaidi ya Bilioni 400 pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa ya Mwanza Isaka." Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. David Kafulila.

Mhe. Wilson Shimo, Mkuu wa Wilaya ya Geita amemuomba Mgeni rasmi kusaidia fedha za kukamilisha Miradi ya maendeleo ya Zahanati na umaliziaji wa vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwenye vijiji vya wilayani Geita.

"Barabara yetu ya kutoka Geita kwenda Nyang'hwale ilikua imewekwa kwenye mpango wa kujengwa kwa kiwango cha lami lakini hazijawahi kutoka fedha za Ujenzi huo na tunateseka" Mbunge wa Nyang'hwale Hussein Amar.

Mbunge wa Busanda ameomba kujengewa Barabara ya Geita-Kahama ambayo inapita kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo na amebainisha kwamba umeme kwenye maeneo mengine haupo ambapo gharama za Uchimbaji zinakua kubwa kutokana na matumizi ya Mafuta ya dizeli kuendeshea mitambo.

Naye, Mbunge wa Mbogwe Mhe. Maganga amesema wachimbaji wadogo bado wana changamoto ya kuwezeshwa kwenye kujikwamua na Uchumi.

Salamu kutoka TCCIA Mkoa wa Geita zilizowasilishwa na Bi. Betha Komba zimebainisha kuwa uratibu wa masuala mbalimbali ya maendeleo kama maonesho ya Madini 2021 yamejenga umoja na ushirikiano baina ya wafanyabishara na Serikali.

Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo (GEREMA), Christopher Kadeo amesema wao kama wachimbaji wadogo wana changamoto ya mitaji ya kuendesha biashara zao hivyo ameziomba taasisi za kifedha kuwasaidia kupata mikopo ya kuendesha biashara zao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho Ndugu James Chiragi amesema lengo kuu la maonesho ya Madini 2021 ni kuonesha teknolojia na kutangaza fursa za biashara na kuwakutanisha wachimbaji wakubwa na wadogo ili kuboresha shughuli za Uchimbaji na kuwakutanisha wadau wa uchimbaji na taasisi za kifedha kwa ajili ya kuwaunganisha ili waweze kupata mikopo ya kuendesha shughuli zao.

"Napenda kutambua mchango wa mdhamini Mkuu ambao ni kampuni ya GGML pamoja na wengine walioshirikiana na mdhamini Mkuu kwa mchango wao kwa kipindi cha miaka 4 uliofanikisha kufanyika kwa maonesho haya." Amefafanua mwenyekiti.

Paul Zahoro

Geita RS.







Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC MURAGILI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE ROBO YA TATU (Januari-Machi 2024/2025)

    May 08, 2025
  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkutano wa baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya 3 kwa mwaka 2024/2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa