• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mhe.Silinde aipongeza Bukombe kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.

Imewekwa: July 23rd, 2021

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde ameupongeza Uongozi wa halmashari ya Wilaya ya Bukombe kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo yakiwemo madarasa, mabweni, Bwalo la chakula pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami nyepesi yenye urefu wa km 200.

"Kama hapa tu tumekaa kwenye bwalo, hii pekee yake inatosha kuniambia kuwa nikienda kwenye mabweni mambo ni mazuri. Hongereni sana."

Pongezi hizo amezitoa tarehe 22 Julai, 2021 akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe.

Aidha amesema changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa ni janga la kitaifa hivyo Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekwishatoa kiasi cha shilingi Bilioni 125 kwa ajili ya kumalizia maboma 10,000 na ametafuta fedha nyingine kwa ajili ya shule 1000 mpya za sekondari.

" Katika shule mpya 1000 awamu ya kwanza tutajenga shule 300, awamu ya pili shule 400 na awamu ya tatu tutamalizia kwa shule 300."

Mhe.Silinde amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Saidi Nkumba kuendelea kuwahamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kuanzisha maboma pamoja na uanzishaji wa majengo ya shule mpya.

"Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ina historia nzuri ya ufaulu mzuri wa shule za msingi hakikisheni mnaanzisha maboma pamoja na shule mpya za sekondari ili watoto wetu wapale mahali pazuri pa kujifunzia."

Vile vile Mhe.Silinde amemtaka Meneja wa TARURA Wilaya ya Bukombe Eng.Africano Orota kuhakikisha anasimamia vizuri ujenzi wa barabara ili kutomkatisha tamaa Mhe.Rais.

"Kwa upande wa barabara Mhe.Rais ametoa fedha moja kwa moja kwa kila jimbo awamu ya kwanza Milioni 300 na awamu ya pili Bilioni 1. Mkasimamie vizuri ili tusimkatishe tamaa Mhe. Rais ili mwaka mwingine wa fedha aweze kutupatia fedha nyingi zaidi."

Akisoma taarifa fupi ya Wilaya ,Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Said Nkumba amesema halmashauri ya Wilaya ys Bukombe inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, vifaa vya maabara, nyumba za walimu, walimu wa sayansi kwa shule za sekondari na walimu wa shule za msingi.

 Aidha ameiomba Serikali ya awamu ya sita kuendelea kuajili walimu wa kutosha ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa walimu kwa shule za msingi na waalimu wa sayansi kwa shule za sekondari.

Mhe.Naibu Waziri akiwa Wilayani Bukombe amekagua miundombinu ya shule ya sekondari Bukombe yakiwemo madarasa, Mabweni, Bwalo la chakula pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami nyepesi Ushirombo Mjini.






Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa