• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mil 400 kujenga miundombinu kituo cha afya Uyovu wilaya ya Bukombe

Imewekwa: March 8th, 2018

Halmashauri ya wilaya ya Bukombe imepokea jumla ya Tsh.400,000,000/= kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kupitia udhamini wa Benki ya Dunia kwa ajili ya maboresho ya Kituo cha Afya Uyovu ili kiweze kutoa huduma ya upasuaji wa dharula kwa kinamama wajawazito. Hii ikiwa ni awamu ya pili ya mpango wa serikali wa maboresho ya vituo vya kutolea huduma za Afya.

Fedha hizi zimelenga kujenga Wodi ya Wazazi (Maternity ward) 1, Wodi ya Watoto (Paediatric ward) 1, Maabara (Laboratory) 1, Nyumba ya Mtumishi (Staff House) 1, Jengo la Kliniki ya Baba, Mama na Mtoto (Reproductive and Child Health Clinic (RCH) ) 1.

Fedha hizo pia zitatumika kujenga chumba cha kuhifadhia Maiti (Mortuary room) 1, njia ya kupitia kuunganisha wodi na Theatre (Walkway) na kukarabati jengo la Upasuaji (Theatre) 1, jengo la kufulia nguo (Laundry).

Zoezi la ukarabati wa kituo cha Afya Uyovu limeanza rasmi mwishoni mwa mwezi Januari mara baada ya Bodi ya Zabuni ya Halmashauri na Kamati ya fedha, Uchumi na Mipango kuridhia matumizi ya pesa hizo kwa mfumo wa "Force akaunti" yaani kutekeleza mradi huo kwa kutumia mafundi wa jamiiili kuweza kupata thamani halisi ya pesa iliyotolewa.

Katika kuhakikisha ujenzi wa miundombinu hii ya afya inakuwa katika kiwango cha ubora wa hali ya juu,Kamati ya ujenzi ambayo wajumbe wake ni wananchi wa kata ya Uyovu wakishirikiana na wataalamu kutoka Halmashauri kushiriki katika ujenzi huo kwa kufyatua matofali katika kituo hicho ili kuweza kudhibiti ubora wa tofalil zinazotumika katika ujenzi pamoja na uimara wa majengo yanayojengwa.

Hatua mbalimbali za ujenzi wa miundombinu hii imefikiwa ambapo Wodi ya watoto ipo hatua ya kufungwa mkanda kwenye madirisha,jengo la maabara lipo hatua ya usawa wa lenta,Nyumba ya mtumishi ipo hatua ya usawa wa kufunga lenta ya mwisho,jengo la kliniki ya baba mama na mtoto limefikia hatua ya kufunga mkanda wa Madirisha.

Kituo Cha Afya Uyovu kinahudumia wananchi takribani elfu 92,464 idadi hii ambayo haiendani na uhalisia wa huduma zilizopo kwani inawalazimu wagonjwa wengine kupelekwa Hospitali ya wilaya ambayo ipo umbali wa kilomita 46 ili kupatiwa huduma.

 Hii imepelekea Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutenga na kupeleka fedha kata ya Uyovu ili kuboresha huduma za Afya na kusogeza huduma hiyo karibu zaidi na wananchi.

Ujenzi wa Jengo la Nyumba ya mtumishi lipo hatua ya usawa wa kufunga lenta ya mwisho.

Ujenzi wa Jengo la Wodi ya watoto kata ya Uyovu umefikia hatua ya kufungwa mkanda kwenye madirisha.

Ujenzi wa Jengo la maabara Kituo cha Afya Uyovu lipo hatua ya Lenta.

Ujenzi wa Jengo la kliniki ya Baba ,mama na Mtoto limefikia hatua ya kufunga mkanda wa Madirisha.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa