• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Milioni 141 chenji ujenzi wa madarasa Bukombe.

Imewekwa: December 29th, 2021

Leo Disemba 29, 2021 Halmashauri ya wilaya ya Bukombe imekabidhi Madarasa Mapya 107 yenye thamani ya Bilioni 2.1 chini ya Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19 kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemery Senyamule.

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye shule ya Sekondari Katente, Mhe. Senyamule ameupongeza uongozi wa Wilaya hiyo kwa Usimamizi uliofanikisha kukamilisha ujenzi wa Madarasa kwenye ubora unaokusudiwa.

Aidha, amewapongeza kwa uadilifu na uaminifu wa kubana matumizi uliopelekea kubakisha fedha kiasi cha Tshs. Milioni 141.5 kwenye manunuzi na Ujenzi wa Madarasa hayo chini ya usimamizi wa viongozi ngazi ya Wilaya, Halmashauri na wakuu wa Shule kwa kushirikiana na kamati za ujenzi.

"Naomba niwahakikishie ndugu wananchi, majengo haya yana ubora unaokusudiwa, kamati mbalimbali za Mkoa na Halmashauri zimepita kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa haya kuanzia kwenye ngazi za awali kabisa ya Ujenzi hadi kufikia hapa." Mkuu wa Mkoa.

"Hongereni sana Bukombe, hii ni miongoni mwa wilaya ambayo imefanya vizuri sana, naomba tusije baada ya mwaka mmoja tukute darasa limekua na rangi ya maziwa badala ya nyeupe, walimu mna kazi kubwa kuwaelekeza wanafunzi kutunza madarasa haya tuwafundishe maadili na uzalendo ikiweno kulinda rasimali." Mkuu wa Mkoa.

"Nipongeze leo nimepanda mti wa matunda wa mparachichi kwenye uzinduzi huu, jambo hili limenikumbusha jambo moja kwamba chakula bora ni pamoja na matunda hivyo basi shule zote tunao wajibu wa kupanda miti ya matunda ili kuboresha lishe kwa wanafunzi." Senyamule.

Vilevile, Mhe. Mkuu wa Mkoa ametembelea na kuona madarasa yaliyokamilika kwenye shule za Sekondari Runzewe, Msasa, Businda ambapo amepongeza juhudi kubwa iliyotumika kukamilisha ujenzi wa madarasa kwenye shule hizo ambao utasaidia kupunguza msongamano kwa wanafunzi madarasani.

"Mhe. Mkuu wa Mkoa, kwenye mradi huu Wilaya ya Bukombe tutabakiza fedha Tshs. Milioni 141.5 na fedha hizi zote zilizobaki zitaombewa kibali maalum cha kuzitumia kwenye maeneo ya shule husika." Amesema Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Mhe. Said Mkumba.

Katika nyakati tofauti, Mwenyekiti na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe wamewawashukuru na kuwapongeza watumishi, wadau na wananchi wote walioshiriki kufanikisha Bilioni 2.1 zinatumika kama ilivyokusudiwa.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Rosemary Senyamule amefanya ziara kwenye mradi wa Maji Nampahalahala unaogharimu Tshs. Bilioni 1.1 ambao mwezi Januari 2022 utakapokamilika utahudumia wananchi 6,108 kwa kuwapatia maji safi na salama na kuwaepusha na kupata maradhi ya kuhara, Kipindupindu na homa ya matumbo.

Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema chanzo hicho cha Maji kinapaswa kulindwa kwa kupanda miti ili maji hayo yaweze kuongezeka kutokana na uwepo wa uoto wa asili pamoja na miti ya kupandwa.

Paulo Zahoro

Geita RS.


Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa