• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MKANDARASI ATAKIWA KUKAMILISHA MRADI WA MAJI KWA WAKATI-MENEJA RUWASA

Imewekwa: February 11th, 2024

Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA Mkoa wa Geita Mhandisi Jabiri Kayilla amemuagiza Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Maji Namsega uliopo Wilayani Bukombe kuhakikisha anakamilisha mradi huo kwa wakati ili uanze kutoa huduma kwa wananchi.

"Mradi huu tunatarajia kuukabidhi kwa wananchi ifikapo tarehe 30 Februari, 2024. Ninamuagiza Mkandarasi  kufanya ukamilishaji wa maeneo madogomadogo yaliyobaki ili mradi uanze kufanya kazi."

Maagizo hayo ameyatoa tarehe 10 Februari, 2024 wakati wa ziara ya kutembelea mradi huo uliohusisha Mameneja wa Maji Wilaya, Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji, Wakurugenzi wa Mabonde ya ziwa Tanganyika na ziwa Victoria na Maafisa wa Ubora wa Maji Kanda ya ziwa.

Akisoma taarifa ya mradi huo Meneja RUWASA Wilaya ya Bukombe  Mhandisi James Benny alisema mradi wa maji Namsega unatekelezwa na Mkandarasi  Yajuk Investment Co Ltd kupitia Programu ya Malipo Kulingana na Matokeo.

Aidha aliendelea kusema kuwa  mradi huo umehusisha ujenzi wa "Power house",  Uunganishaji wa umeme wa gridi, ufungaji wa Pampu ya kusukuma maji, ujenzi wa tanki la maji pamoja na ujenzi wa vituo 12  vya kuchotea maji.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Runzewe Magharibi Mhe.John Nguhi ametoa wito kwa wananchi wa eneo lake kuhakikisha wanatunza na kulinda miundombinu ya maji ili iweze kuwa endelevu na kutoa huduma bora kwani kwa kufanya hivyo huduma ya maji safi na salama itakuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na cha baadaye.

Jumla ya wananchi12,850 na vijiji 3 ambavyo ni Namsega, Kazilamuyaye na Msangila watanufaika na mradi wa maji Namsega wenye thamani ya shilingi 954,778,618.69.


Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa