• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mkoa wa Geita Waadhimisha Siku ya Mazingira Duniani

Imewekwa: June 5th, 2021

Mkoa wa Geita waadhimisha Siku ya mazingira Duniani kwa kuzindua mradi wa kuotesha Miche ya miti kwa shule za Msingi na Sekondari. Mhe. Said Nkumba, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita amezindua Mradi wa Uoteshaji Miti kwenye shule za Msingi na Sekondari mkoa Geita ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Wilayani Chato leo Juni 05, 2021.

Akizungumza na wananchi, Mhe. Nkumba ametoa wito kwa viongozi kufanya suala la uhifadhi wa mazingira kuwa ajenda ya kudumu na amewapongeza TFS kwa utayari wa uhifadhi kwa kutoa utaalamu na huduma kwenye uoteshaji wa miti na uhifadhi kwa ujumla

."Sote kwa pamoja, tupande miti mingi wakati wa mvua ili kujinususuru na jangwa na mabadiliko ya tabia nchi,"amesema.

Aidha, Mhe. Said Nkumba ametoa onyo kwa wanaokata miti kwa Shughuli mbalimbali zikiwemo za Uchimbaji wa Madini (Matimba) kuacha mara moja tabia hiyo badala yake watumie teknolojia zingie rahisi kwani wanahatarisha afya ya kila mmoja na kuharibu uchumi

.Awali, akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Buseresere na Shule ya Msingi Bwanga wakati akikagua vitalu vya miti, Mhe. Nkumba ametoa wito kwa wanafunzi kufikisha Elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa Wazazi wao waweze kutunza miti ya asili ambayo pia ina faidi nyingi kwenye maisha yao ikiwemo kuwapatia mvua, hewa Safi pamoja na ufugaji nyuki kwa kuweka mizinga.

Mhe. Nkumba amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Chato kwa usimamizi imara kwenye masuala ya mazingira hata kupata walimu hodari wa Mazingira waliowapa uwezo  wanafunzi hadi kuwa miongoni mwa wahifadhi kwa kupanda miti na amesema hiyo ni ajira wanaweza kupanda miti ya mbao ambayo inasaidia kuwainua kiuchumi.

Mhe. Fadhil Juma, Mkuu wa Wilaya ya Geita, ametoa rai kwa wataalam kutoa Elimu kwa jamii juu ya utunzaji wa mazingira huku akiwataka wachimbaji kuiga mfano kwa migodi inayotumia zege kushuka na kupanda kwenye mashimo ya Uchimbaji wa madini.

Wakati huohuo, Bi. Sania Mwangakala, kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa ameonya tabia ya ukataji miti hovyo kwa Shughuli za Uchimbaji madini Mkoani Geita.Akitoa ufafanuazi, Kaimu Mkuu wa Idara ya Uzalishaji na Uchumi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,

Mhandisi John Kulola amebainisha kuwa Halmashauri zote za Mkoa wa Geita zimetekeleza agizo la Ofisi ya Makamu wa Rais la kupanda miti isiyopungua Milioni 1.5 na ametoa wito kwa Halmashauri zilizo nyuma kwenye suala hilo kuongeza bidii.Aidha, amebainisha kuwa Usafi wa mazingira ni miongoni mwa kazi kubwa inayofanywa na Mkoa wa Geita pamoja na upandaji miti kwenye maeneo yote hususani kwenye migodi.

Vilevile, Ndugu Kulola amefafanua kuwa utumiaji wa Nishati mbadala ni miongoni kwa mkakati wa Mkoa na ametoa wito kwa wanaojihusha na Shughuli za Uzalishaji matofali watumie pumba za mpunga badala ya kuni ili kuendelea kuhifadhi mazingira.Mwanafunzu Juma Magesa,

 Mwenyekiti wa Club ya Malihai Chato Sekondari amesema kuwa, wao kama wanafunzi wanatoa Elimu kwa wenzao ambao wapo nje ya Club ya mazingira nao pia wanapeleka ujumbe kwa wazazi nyumbani juu ya faida za upandaji miti na kuhifadhi mazingira.Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka 2021 inasema "Tutumie nishati Mbadala kuondoa mfumo wa Ikolojia"

.#KaziIendelee




Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa