• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mkuu wa Mkoa wa Geita kuimulika Wilaya ya Bukombe

Imewekwa: September 10th, 2022

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Geita kuimulika wilaya ya Bukombe-Ushirombo

Mkuu wa wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Reuben Shigela afanya ziara ya utambulisho Mkoani Geita wilayani Bukombe katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya mnamo tarehe ……huku akisisitiza viongozi kupendana na kufanya kazi kwa ushirikiano .

Akizungumza na vyombo vya habari RC Shigela ameeleza kuwa anayofuraha kubwa kuwa mkuu wa mkoa wa Geita na kumshukuru sana Mh.Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu huku akiliweka mbele suala zima la Ushirikiano.

‘‘Niwasalimu kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Pongezi zangu  ziende kwa Mh.Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan,Mh.Mkuu wa wilaya ya Bukombe,Mkurugenzi wa wilaya ya Bukombe,Ndugu Viongozi wa idara ya ulinzi ,Ndugu Madiwani na Viongozi wengine nipende kuwaasa viongozi wenzangu tufanye kazi kwa ushirikiano ili kuiendeleza wilaya hii’’ 

Aidha Martin Shigela, Alieleza kuwa Mkoa wa Geita ni Mkoa wenye Ajenda ya maendeleo na kutoa pongezi kwa wilaya ya Bukombe ambayo hivi karibuni imeendelea kufanya vizuri katika shughuli za maendeleo kutokana na ongezeko la Ubora wa miundombinu pamoja na usimamizi wa miradi ya wilaya kwa umakini zaidi.

‘‘Mkuu wa wilaya pamoja na jopo lako napenda kuwa pongeza kulingana na kazi kubwa mnayo ifanya kwani jitihada zenu zimekuwa zikionekana kwani ndiyo matunda  yanayotegemewa na wananchi hivyo nipende kuwapa pongezi zangu za dhati na muendelee na moyo huo huo’’Ametolea ufafanuzi Zaidi,

Hata hivyo  Shigela alisisitiza Madiwani wa kata,Watendaji pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali kufanya kazi kwa mshikamano na kuweka weredi wao katika  ukusanyaji  Mapato na kuepuka kutumia hovyo rasilimali za kiserikali huku wakisingizia sababu mbalimbali zisizo na umuhimu.

‘‘Ushirikiano katika ukusanyaji wa Mapato na matumizi katika Ngazi ya Kata na Wilaya kwa ujumla ni vyema kufanywa na viongozi wote ili kuhakikisha usalama wa fedha za Serikali na matumizi sahihi ya fedha hizo’’  alieleza,

Akihitimisha hotuba yake fupi katika ziara hiyo  Shigela aliwaasa viongozo wa Ngazi zote kuhakikisha wana wapatia wananchi elimu ya kutosha kuhusu Sensa ya watu na makazi na kuhakikisha  makalani fedha zao wanagawiwa kwa mpangilio uliokuwa sahihi.

‘‘Kwa kumalizia hotuba yangu nipende kuwaomba Waheshimiwa viongozi kwa pamoja tushikamane kuhamasisha suala la Sensa linaenda sawia na mfanye mgao uliokuwa mzuri katika fedha za Makalani’

Na,Kwa upande wake Mh.Mkuu wa wilaya Said Nkumba  alimpongeza Mkuu wa mkoa Martin Shigela kwa kupanga ziara hiyo na kufanikisha hotuba yake yenye  tija katika Wilaya yake na kuahidi kutoa ushirikiano katika utendaji kazi na kuwaasa viongozi waliochini yake kumuunga mkono.

‘‘Nipende Kumshukuru Mkuu wa mkoa kwa jitihada na moyo wa upendo dhidi ya wana Bukombe na nikuahidi kwamba sisi kama wana Bukombe tuna ahidi kushirikiana nawe Bega kwa bega na niwaombe Ndugu viongozi wenzagu tushirikiane na tuache chokochoko zisizo na maana kwa ajili ya maendeleo ya wilaya yetu kwa ujumla’’ alieleza

Hata hivyo katika kuhitimisha kikao kilichotokana na ziara ya Mkuu wa Mkoa naye Diwani wa kata ya Runzewe mashariki  Mery Nchiba alitoa yake ya moyoni huku akiahidi kushikamana na madiwani pamoja na viongozi wenzake katika kuhakikisha wanalinda Nyara za serikali na kusimamia vema ukusanyaji mapato.

‘‘Namshukuru Mh.mkuu wa wilaya pamoja na mkuu wa mkoa kwa ushirikiano wanao tuonesha kwani kwetu ni jambo la pekee kujivunia bila kusita niseme kuwa tunaahidi kumuunga mkono katika kuhakikisha maendeleo yanasonga mbele katika kata zetu na wilaya kwa ujumla bila kusahau kumpa kongole Mbunge wetu Dotto Biteko kwa kazi kubwa anayoifanya’’Alibainisha Diwani kata ya Runzewe Mashariki

Pia Diwani huyo aliendelea kusema kuwa kuhusu suala la Sensa kushirikiana na Waheshimiwa viongozi wenzake watalisimamia kinaga ubaga kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu sahihi kuhusu uandikishwaji wa sensa ya watu na makazi kuanzia ngazi za kata hadi wilaya kwa ujumla kwa kushirikiana Mkuu wa wilaya hiyo Said Nkumba.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa