• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Nape Nnauye ahaidi kupanda nyasi uwanja wa michezo Wilayani Bukombe- Kilimahewa

Imewekwa: September 11th, 2022

Waziri wa habari, mawasiliano na tekinolojia ya habari Mhe. Nape Nnauye ameahidi kupanda nyasi uwanja wa michezo unaomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kwa kuweka nyasi pamoja na kutengeneza eneo kwaajili ya viongozi na mashabiki watakao kuwa wakihudhuria mashindano mbalimbali uwanjani humo.

Ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi zawadi katika mashindano ya  fainali ya Doto cup yaliyofanyika katika uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe- Kilimahewa.

"Kutokana na mchezo mzuri na hamasa nzuri niliyoikuta hapa, Mimi na Mhe. Doto  Biteko tutapambana na  tutahakikisha mashindano yajayo ya Doto cup ya mwaka 2023 uwanjani hapa patakuwa na nyasi, lakini pia tutatengeneza maeneo kwa ajili ya kukaa viongozi na mashabiki watakao hudhuria mashindano hayo" amesema Mhe. Nape Nnauye.

Aidha Mhe. Nnauye amewataka vijana kuwa na tabia ya kufanya mazoezi Mara kwa mara na kutumia vipaji vyao kujiajiri.

Nae Waziri wa madini na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto  mashaka Biteko ambaye pia ni mdhamini wa mashindano hayo amemshukuru Mhe. Nape Nnauye pamoja na viongozi wote waliohudhuria fainali ya Doto cup 2022.

Pia amewapongeza washindi na washiriki wote wa Doto  cup bila kuisahau kamati ya maandalizi ya mashindano ya Doto cup 2022 kwa kazi nzuri waliyoifanya hadi kukamilika kwake.

"Nawashukuru sana wote mliohusika kuandaa zoezi hili, nyie ndio mnajua kilakitu kuhusiana na maandalizi yote ya mashindano, inaonesha jinsi gani watu wa Bukombe ni welevu na wachapa kazi." Amesema Mhe. Biteko.
Dr. Biteko ameomba ushirikiano na uchapa kazi huo kwa vitendo uendelee na uwe tamaduni ya wana Bukombe siku zote.

Fainali ya Doto cup iliambatana na michezo mbalimbali  ikiwemo mashindano ya kukimbiza kuku, mbio za mita mia moja, kuvuta kamba, kukimbia na magunia, kaleti, mpira  wa Pete pamoja na mpira  wa miguu ambapo timu iliyochukua ubingwa katika mpira wa miguu ilikua ni timu ya Butinzya scorpion football club.

Zawadi zilizotokewa kwa mshindi wa kwanza ambapo ni timu ya Butinzya scorpion football club ilikua ni fedha taslim za kitanzania shilingi milioni moja, jezi kamili seti tatu pamoja na mipira mitatu. Mshindi wa pili ambapo ni timu ya Runzewe Academy Walijipatia fedha taslim za kitanzania shilingi laki tano, seti kamili za jezi mbili, pamoja na mipira mitatu, na kwa mshindi wa tatu ambapo ni timu ya Warrior ushirombo  ilijipatia fedha taslim shilingi laki moja, Seti kamili ya jezi pea moja pamoja na mpira mmoja. Aidha washindi wa timu zote tatu walizawadiwa medali kwa kila mshiriki.

Afisa michezo Wilaya ya Bukombe, Jenipha Kisusi alisema halmashauri imejipanga kutunza miundombinu ya uwanja ikiwa ni miongoni mwa vyanzo vya mapato ya ndani.

Kisusi aliwaomba wananchi kupenda mazoezi hali ambayo itawasaidia kuimarisha mwili na afya zao na kuweza kuepuka magonjwa nyemelezi.

Mwisho.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa