• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Nimekuja Hapa Kutatua Changamoto Zenu Wanabukombe

Imewekwa: June 6th, 2021

#Nimekuja hapa na timu nzima ya Wizara kwa ajili ya kutatua changamoto zenu.

#Mhe Doto Biteko anazijua changamoto zenu na ndo maana ametuleta hapa ili tuzitatue na hii ndo faida ya kuwa na Mbunge anayejua shida za wananchi anaowaongoza na kujua wapi azipeleke ili zipate majibu

#Tumekuja katika hali ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo inatutaka kuongeza ushirikiano kati ya Hifadhi na Wananchi.#Ombi la wananchi kutoondolewa katika pori la Kigosi tumelipokea na hakuna Mfugaji wa Nyuki atakayeondolewa

#Tutaweka utaratibu wa kugawa maeneo kwa vikundi ili mfugie humo na tutaanzisha utalii wa nyuki ili muweze kupata na fedha kutokana na utalii huo

#Wizara imejenga kiwanda cha kisasa Bukombe ambapo tutaleta mashine ya kuchakata asali na Bukombe tutazalisha asali bora ya kwanza Tanzania nzima.

#Naomba tuendelee kumuunga mkono Mbunge wetu maana ni wabunge wachache sana ambao wanatekeleza wajibu wao kwa wananchi kwa kiwango hiki kikubwa na ndiyo maana tumefika hapa

WAZIRI WA MADINI NA MBUNGE WA JIMBO LA BUKOMBE: MHE DOTO BITEKO.

#Nawashukuru sana watu wa Bukombe kwa kuacha kazi zenu na kuja kutusikiliza na leo ni Jumapili kwani mgeweza kupumzika nyumbani  lakini mmetuheshimu na kuja kwa wingi. Asanteni sana na Mungu awabariki sana.

#Namshukuru sana Mhe. Damas Ndumbaro Naibu Waziri na watendaji wote wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuja hapa Bukombe

#Suala la kutolewa katika msitu kwa wafugaji wa nyuki ni changamoto kwetu na ndo maana tunaye Waziri mwenye dhamana.#Mhe Ndumbaro tunaomba ulete matumaini na faraja kwetu. Asilimia kubwa ya eneo la Bukombe ni hifadhi hivyo mahusiano yetu watu wa Bukombe na Hifadhi ni ya muhimu sana.

#Ndugu zangu watu wema wa Bukombe, Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ameendelea kutuunga mkono kwa kutupatia fedha za maendeleo katika sekta za Afya, Elimu, Maji na Barabara ambapo miradi mingi inaendelea kujengwa na pia tumepata magari mawili ya wagonjwa ambapo moja litaenda Namonge na jingine Bulega.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII : MHE MARY FRANCIS MASANJA

#Nawapongeza sana watu wa Bukombe maana mmepata mbunge mahili, msikivu na anayewapenda.#Mhe Biteko amekuwa akitusumbua na kutaka tuje hapa kutatua kero zenu na ndo maana tumefika.

#Mhe Biteko ni Lulu, mg'ang'anieni maana mkimuacha maeneo mengine wanamhitaji

#Bukombe mmekuwa mfano mzuri kwa ufugaji wa nyuki na mnazalisha asali bora. Naomba pia muendelee kuhifadhi mazingira.

MKUU WA WILAYA YA BUKOMBE : MHE SAID NKUMBA

#Ujio wa ugeni huu ni kutokana na mualiko wa Mbunge wetu Mhe. Biteko maana amesikia kero zetu na leo tunaye Waziri, Naibu Waziri na watendaji wa Wizara hii. Sio jambo la kawaida Wizara nzima kufika hapa.#Tunakushukuru sana Mheshimiwa Biteko

MWENYEKITI WA CCM (W) BUKOMBE DANIEL MACHONGO

#Hongera Mhe. Doto Biteko kwa jinsi anavyoshughulikia changamoto zinazowakabili wananchi na umedhihirisha ni kwa namna gani anawajali wananchi wako

#Nawaomba wanabukombe muendelee kumuunga mkono Mbunge wenu.

Imetolewa na:-

Kitengo cha TEHAMA.

Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

Tarehe 06 Juni, 2021.



Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa