• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RC Geita awataka Wakurugenzi kufufua kamati za UKIMWI ngazi ya Vijiji,Mtaa na Kata.

Imewekwa: December 1st, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kufufua Kamati za UKIMWI ngazi ya Vijiji, Mitaa na Kata na utendaji wa Kamati hizo pamoja na kutenga Bajeti kwa ajili ya Utekelezaji wa jukumu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kundi hilo linahudumiwa vizuri.

Mhe. Senyamule amesema hayo leo Disemba 01, 2021 wakati alizungumza na wananchi kwenye viwanja vya Uyovu Wilayani Bukombe wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani Mkoa wa Geita.

Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa amewataka Viongozi na wanachama wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi (KONGA) kuendelea kuhamasisha WAVIU wajiunge na KONGA na kuwa wafuasi wa dawa za kufubaza makali ya VVU na kufuata maelekezo yanayotolewa na watoa huduma za afya majumbani na wataalamu wa afya ikiwemo kuzingatia elimu ya lishe bora.

Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi dhidi ya janga la Ugonjwa wa Uviko 19.

"Napenda kuwahamasisha kutafakari kwa kina na kwa hiari kupokea chanjo dhidi ya Ugonjwa wa Uviko 19 na kutumia njia zote za kujikinga zinazotolewa na wataalamu wetu wa Afya," amesema.

Akisoma taarifa ya Mkoa ya hali ya Utekelezaji wa shughuli za mapambano dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Ndugu Elikana Haruni amesema jumla ya watu 175,206 (Wanawake 107,382 sawa na asilimia 61 na Wanaume 67,824 sawa na asilimia 39) walichukuliwa sampuli ya damu katika vituo na mikusanyiko mbalimbali kwa ajili ya kupimwa maambukizi ya VVU.

 Kati ya hao, watu 10,823 (sawa na 6% ya wote waliopimwa) walibainika kuwa na maambukizi ya VVU. Kati ya hao Wanawake walikuwa 6,284 (sawa na 58%) na Wanaume walikuwa 4,539 (sawa na 42%).

"Kwa mama wajawazito, jumla ya wajawazito 107,961 walipatiwa huduma ya ushauri nasaha na kupimwa VVU katika hudhurio la kwanza Kliniki. Kati ya hao, akina mama wajawazito 739 (sawa na asilimia 0.7%) waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU na kuanzishiwa dawa za kufubaza makali ya VVU (ARVs)." Amesema Haruni.


Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa