• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Rc Senyamule:''Tufanye mapinduzi ya kiuchumi''

Imewekwa: September 4th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule amewaagiza Wakuu wa Wilaya kuwa na mipango thabiti ya kutumia Kilimo, Uvuvi na Ufugaji wa kisasa ili kuongeza tija kwenye uzalishaji ili kuongeza mapato ya Halmashauri hatimaye kuwainua wananchi kiuchumi.

Akizungumza leo septemba 03, 2021 kwenye kikao cha Kimkakati kilichoketi mahsusi kujadili namna bora ya kuinua Mkoa kwenye mapato kuendana na uboreshaji wa huduma kwa jamii ambapo kimewakutanisha viongozi wa Wilaya na Halmashauri za Mkoa wa Geita, Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa siku 90 kwa viongozi hao kurudi na mpango wa kusaidia wananchi.

"Tufanye Mapinduzi ya Kiuchumi, zipo fursa za Kilimo, Uvuvi, Mifugo ambazo hazijafanyiwa kazi ipasavyo sasa twendeni tukaweke mikakati ya pamoja ya kufanya Mapinduzi ya Kiuchumi." Amesisitiza Mkuu wa Mkoa.

Vilevile, Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa viongozi hao kusimamia taratibu za kutoza ushuru na tozo kwenye Shughuli za Uchimbaji Madini ili mapato ya ndani kutokana na Shughuli hizo yasiwe kandamizi na tozo ziende kwenye uboreshaji wa Miundombinu ya Shughuli husika ili ziwanufaishe walio kwenye sekta hiyo.

Mhe. Senyamule amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa nia ya dhati ya kuinua sekta ya Elimu nchini ambapo siku za karibuni Mkoa wa Geita umepokea fedha za kujenga zaidi ya madarasa 1400 na amewaagiza Wakurugenzi kuratinu na kusimamia kwa umakini mkubwa ili Miradi hiyo iishe kwa wakati na ubora unaokusudiwa.

Hata hivyo Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa viongozi hao kuwa na mkakati wa kumaliza changamoto ya madarasa na vyumba vya madarasa kwa kutumia vyanzo vya ndani pasipo kusubiri fedha kutoka serikali kuu kwani tatizo la Msongamano wa wanafunzi bado ni kubwa Mkoani Geita.

Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa amewapongeza viongozi hao kwa juhudi kubwa zilizopelekea kuwa na 92% ya uwepo wa vituo vya kutolea huduma za Afya na ameagiza idara hiyo kupeleka Watumishi kwenye Zahanati 32 mpya zilizokamilika ili ziweze kutoa huduma kwa wananchi na kukamilisha Miundombinu ya Zahanati 105 zilizo kwenye hatua mbalimbali ya ujenzi.

Akiwasainisha Wakuu wa Wilaya Mikataba mipya ya Miaka Mitano ya Utendaji kazi na Usimamizi wa Shughuli za Lishe, Mhe. Mkuu wa Mkoa amewataka Maafisa Lishe kwenye Halmashauri zote kusimamia vema Shughuli za Lishe kama wanavyosimamia programu zingine za serikali ili kufikia lengo la Taifa la kuiokoa jamii kutoka kwenye udumavu unaofifisha juhudi za ukuaji wa Uchumi.

Mhe. Mkuu wa Mkoa amesisitiza ukusanyaji wa Mapato kufuata Sheria na taratibu za fedha ikiwa ni pamoja na matumizi ya Vifaa maalumu vya kukusanyia mapato (POS) na sio vinginevyo ili kuzuia upotevu wa Mapato.

Hata hivyo ,Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Vijiji akawaagiza kutatua kero za wananchi kwa wakati ili kuisaidia jamii kwani hoja nyingi ni za kawaida na wanahitaji msaada wa haraka.

 

Baada ya wito wa kufuata taratibu zinazoshauriwa na wataalamu wa Afya katika kupambana dhidi ya Ugonjwa wa Uviko 19 ikiwa ni pamoja na Chanjo ya Ugonjwa huo, Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa Viongozi kuendelea na maandalizi ya Shughuli ya Kitaifa ya Kukimbiza na Kuzima Mwenge Maalumu wa Uhuru 2021 inayotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba pamoja na Maonesho ya Nne ya Teknolojia ya Madini na uwekezaji yatakayifanyika kuanzia Septemba 16-26.

Awali, Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji, Ndugu James Chiragi alitoa wito kwa Halamshauri kuhakikisha 20% ya mapato yatokanayo na Kilimo, 15% kutoka kwenye Mifugo na 5% kutoka wenye Uvuvi zirejeshwe kwenye sekta hizo kama Sheria unavyosema ili kuboresha Shughuli za Ugani.

"Unapoongeza thamani kwenye mazao ya Uvuvi, unaongeza mnyororo wa biashara ambapo wananchi wengi watahusika na mwisho tija kwenye zao hilo itaongezeka". Tito Mlelwa, Afisa Uvuvi wa Mkoa.

Afisa Madini Mkazi wa Mkoa, Ndugu Daniel Mapunda amebainisha kuwa zuio la kusafisha Kaboni nje ya Mkoa limekua na faida sana kwenye ukuaji wa sekta hiyo kwani limepelekea ongezeko la 'Elution' kufikia 40 kutoka 15 za siku za nyuma Mkoani Geita.

Akiwasilisha mada, Afisa Elimu Mkoa Anthony Mtweve amefafanua kuwa zaidi ya vyumba vya madarasa elfu 11 vitahitajika ifikapo mwaka 2022 ili kukabiliana matatizo la Msongamano wa wanafunzi kwenye madarasa na kwamba kwa sasa madarasa 8830 yanahitajika.

Paul Zahoro

Geita RS.


Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC MURAGILI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE ROBO YA TATU (Januari-Machi 2024/2025)

    May 08, 2025
  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkutano wa baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya 3 kwa mwaka 2024/2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa