• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Saidi Kalidushi Aridhishwa na Ujenzi wa Miradi ya Uviko-19.

Imewekwa: January 15th, 2022

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Said Kalidushi ameridhishwa na ujenzi wa miundombinu ya madarasa ya elimu msingi na sekondari yaliyotekelezwa na fedha za Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO - 19 huku akiwataka viongozi wa Wilaya ya Bukombe kuhakikisha wanaendeleza desturi yao ya kuwashirikisha wananchi katika kutekeleza miradi ya maendeleo katika miradi mingine inayoendelea kutekelezwa.

"Rai yangu kwa viongozi pamoja na wananchi endelezeni moyo huo huo wa kizalendo mliokuwanao wakati wa utekelezaji wa miradi ya UVIKO - 19 katika kutekeleza miradi mingine ya maendeleo katika halmashauri yenu." Said Kalidushi.

Hayo ameyasema tarehe 14 Januari, 2022 katika ziara ya kamati ya siasa Mkoa wa Geita ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo.

Aidha aliendelea kusema kuwa madarasa ya elimu msingi na sekondari kupitia mradi wa UVIKO - 19 katika halmashauri ya Wilaya ya Bukombe yatasaidia kupunguza msongamano kwa wanafunzi ikiwa ni malengo yakupunguza maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO - 19 nchini.

Akiongea katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Said Nkumba amesema, katika utekelezaji wa Miradi ya UVIKO - 19 tumebakiza chenji ya Milioni 141 hii ni kutokana na moyo wa kizalendo walionao wananchi wa wilaya ya Bukombe kwa kushirikisha nguvu zao katika kutekeleza miradi kama vile kuleta mchanga, mawe, maji, kusomba kokoto, kuchimba msingi pamoja na shughuli za umwagiliaji wa majengo yetu.

Vile vile ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kwa kutoa kiasi cha shilingi Milioni 10.5 kwa ajili ya ukarabati wa machinjio ya Katente baada ya kamati ya siasa Mkoa kuifunga kwa muda machinjio ya Mwalo ambayo mazingira yake yalikuwa yanahatarisha afya za wanananchi tarehe 10 Juni, 2021 wakati wa ziara katika halmashauri hiyo.

"Nawapongeza kwa ukarabati huu kwa kufanya hivyo wananchi wameweza kupata huduma ya machinjio katika mazingira mazuri." Said Kalidushi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto shule na mzazi atakaye kiuka atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.’’Tusiwapeleke watoto kwenye machimbo tuwaache wapate elimu.’’

Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule shikizi Migamba, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya sekondari Bukombe, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya sekondari Ushirombo, ukarabati wa machinjio ya Katente, ujenzi wa vyumba sita vya madarasa shule ya sekondari Msonga na ujenzi wa vyumba kumi vya madarasa shule ya shikizi Idoselo.









Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa