• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

''Serikali ya Samia Suluhu Hassan inasema kuwa wafugaji wa nyuki waendelee kuugia kwenye maeneo ya hifadhi kwa utaratibu wa vibali hadi hapo baadae'' Mhe. Masanja

Imewekwa: September 16th, 2022

Naibu wa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Mary Masanja ameyasema hayo leo akiwa ziarani katika Kijiji cha Azimio kilichopo kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.

Mhe Masanja amefika Bukombe kwa mwaliko wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kufuatia ziara yake jimboni ambapo alibaini kero kubwa ya wafuga nyuki wa Bukombe kutaka kuondolewa kwenye maeneo ya hifadhi huku eneo kubwa la Bukombe likiwa ni hifadhi hali inayofanya upungufu mkubwa wa maeneo ya shughuli za kibinadamu kwa Wanabukombe.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza, Mheshimiwa Marry Masanja amesema kuwa, Serikali ya mama Samia haiwezi kukubali wananchi wake wakapata shida maana inajali sana uchumi wa watu wake na kuwaagiza maafisa Misitu kuhakikisha wanakuwa na mahusiano mazuri na wananchi wanaozunguka maeneo ya hifadhi.

Awali Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini Dkt. #DotoBiteko akimuomba Naibu waziri kwa niaba ya wananchi amesema kuwa watu wa Bukombe wanaiomba serikali hii sikivu waendelee kufugia nyuki katika maeneo ya hifadhi maana wao ni watunzaji wa mazingira na ndio maeneo pekee kwao kwa ajili ya shughuli hii huku akieleza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan hataki watu wawe na kero ndo maana anawatuma viongozi wote kutatua kero hizo.

Katika ziara hii ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, haya ndio yaliyojiri;

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: DKT.MARY MASANJA

#Kwanza nawapa salamu za Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan, amenituma nije hapa kutatua changamoto mliyo nayo kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Pindi Chana.

#Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuendelea kutoa thamani kwa asali ya Bukombe ambapo imejenga kiwanda cha Kuchakata Asali chenye thamani ya Tsh. Milioni 504.

#Hii ni kuonyesha kuwa uchumi wa watu  ni muhimu na ndo maana serikali inataka muendelee kubaki porini kwa kufuata utaratibu wa Vibali mpaka serikali itakapokuja na njia mbadala ya kutenga maeneo mengine kwa shughuli hii.

#Naomba muendelee kuzalisha Asali yenu, na mkishazalisha mkaiuze kwenye kiwanda chetu ili iongezwe thamani na sio kuuza vichochoroni maana mnapunjwa.

#Serikali itaanzisha MANZUKI ili kuongeza uzalishaji wa asali kwa kuepuka uhamishaji wa Mizinga hali inayopelekea uharibifu wa Mazingira.

MKUU WA MKOA WA GEITA: MHE MARTINE SHIGELA

#Nampongeza sana Mbunge wenu Dkt. Doto Biteko ambaye anatumia muda vizuri kuwasikiliza nyinyi na kubaini kero zenu na kuzileta serikalini zipate suluhisho. Kero hii ya Wafuga nyuki pamoja na ile ya Probox ambazo amezipata akiwa ziarani ni kielelezo tosha cha kuwa mlichagua vizuri maana hata Rais alimuamini mpaka leo ni Waziri. Nyie mnajua kulea viongozi

#Kero ya Wafuga nyuki tutapata majibu yake leo,lakini hii ya Probox naomba mnipe muda wa kuishughulikia ili tuimalize muendelee na kazi maana Rais Samia anataka tushughulikie shida zenu.

#Natoa maelekezo kwa watendaji wa serikali wote ndani ya mkoa, waachane na tabia ya kukaa maofsini bali wafanye ziara na waende kwa wananchi kusikiliza kero zao. Wawe na majibu kabla sijaanza ziara ya kusikiliza kero za watu ndani ya Mkoa huu.

MBUNGE WA JIMBO LA BUKOMBE NA WAZIRI WA MADINI: DKT. DOTO BITEKO

#Nawashukuru sana watu wa Uyovu kwa kuja kwa wingi huu katika mkutano wetu na Naibu Waziri wa Maliasili. Wingi wenu huu unaonyesha ni kwa namna gani tunatamani kusikia Wizara hii inasemaje kuhusu kero yetu.

# Naomba Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii utusaidie wananchi wa Bukombe kwa kero yetu hii ya Wafuga nyuki. Hatuna mahala pa kufugia,naamini utatusaidia maana hata Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan hayuko tayari kuona kero hizi.

#Pia tunakuomba Mkuu wetu wa Mkoa usaidie vijana wa Bukombe kutokana na changamoto ya Probox(gari ndogo za kusogeza watu maeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi). Tunaomba ziruhusiwe vijana wengi wamejiajiri huko waendelee na kazi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe Said Nkumba amewaeleza wananchi wa Uyovu kuwa ujio wa Naibu Waziri Bukombe ni kutokana na mawasiliano mazuri kati ya Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Wizara hii kutokana na kero kubwa iliyokuwepo na kuwataka wananchi wa Bukombe kuendelea kumuunga Mkono Mbunge huyu kwani anatekeleza majuku yake ipasavyo kwa wananchi.

Katika ziara hii Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Mary Masanja ameambatana na watendaji mbalimbali wa Wizara hii akiwemo mratibu wa mfuko wa Misitu Tanzania Dkt. Tuli, wakuu wa vitengo vya hifadhi kanda, Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa wa Geita na Wilaya ya Bukombe, wakuu wa Idara mbalimbali.

#KusemaNaKutenda

#Kaziiendelee

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa