• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Siku ya walimu Duniani-Geita.

Imewekwa: October 6th, 2021

"Ni Bukombe Pekee ndo Mnaadhimisha Siku ya Mwalimu Duniani kwa Namna Hii ndani ya Mkoa wa Geita."

Hayo yamesemwa tar.05/10/2021 na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mheshimiwa Rosemary Senyamule ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika kuadhimisha siku ya Mwalimu Duniani ambapo Bukombe imefanyika katika Uwanja wa Sekondari ya Ushirombo iliyoko Wilaya ya Bukombe Mkoani humo.

Maadhimisho haya yaliambatana na kilele cha ligi ya Walimu maarufu kama Mwalimu Doto Cup inayodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mheshimiwa Dkt. #DotoBiteko kila mwaka ikiwa na lengo la kuwaleta pamoja walimu wa Bukombe kwani hukutana na kuzungumzia changamoto zinazowakuta walimu na kuona namna gani zinataftiwa ufumbuzi. Benki ya NMB na CWT pia walishirikiana na Mh Biteko kudhamini ligi hii kwa mwaka huu 2021

Katika maadhimisho haya, Mabingwa wa mshindano wamepata zawadi kwa michezo mbalimbali ikiwemo kukimbiza kuku, kuvuta kamba, kukimbia kwenye magunia pamoja na Mpira wa miguu na pete. Kwa mpira wa miguu na pete washindi wamepata zawadi kama ifuatavyo;

Mshindi wa Kwanza: Tsh milioni 1.2, medali, kombe, mipira 3

Mshindi wa pili: Tsh 700,000/=, mipira 2

Mshindi wa tatu : Tsh 500,000/=, mpira 1

Hii ni pamoja na kutoa zawadi kwa shule zilizofanya vizuri kwa mitihani ya darasa la nne, la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita.

Katika hafla hii, Mkuu wa Mkoa ameambatana na wageni mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Mheshimiwa Nicodemus Maganga,Katibu Mkuu CWT Bwana Deus Seif, Meneja wa NMB kanda Bwana Sospiter Njire akiwa na Afisa Mkuu rasilimali watu NMB, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mh Said Nkumba na kamati ya Ulinzi na Usalama, Mwenyekiti CCM(W) Ndg.Daniel Machongo na kamati yake, Mkurugenzi Mtendaji(W) Bwana Lutengano George na wakuu wa Idara, Mwenyekiti wa Halmashauri Mh Yusuph Mohamed pamoja na Madiwani ,Mkurugenzi Mkuu wa GGM Bwana Johnson akiwa na Simon Shayo makamu wa rais wa mgodi, viongozi wa CWT Mkoa wa Geita na Wilaya mbalimbali, walimu pamoja na mamia ya wananchi waliojitokeza kwa wingi.

Katika hafla hii haya ndio yaliyojiri:

MKUU WA MKOA WA GEITA: MH ROSEMARY SENYAMULE.

#Nakupongeza sana Mheshimiwa Biteko kwa jinsi unavyoendelea kuwakusanya walimu na kufanya jambo kubwa kama hili ambalo umekuwa ukilifanya kila mwaka. Pia nawapongeza NMB kwa kushiriki kudhamini mashindano haya

#Ni wachache sana wanaorudisha shukrani, leo tunashuhudia na sisi tumejifunza Bukombe. Walimu wakitoka hapa wanakuwa vizuri na ndo maana Bukombe mnafanya vizuri kwenye mitihani maana mnapata motisha.

#Ni Bukombe pekee ndo mnaadhimisha siku hii kwa namna hii ndani ya Mkoa wa Geita. Na kupitia hili tumejifunza Bukombe, nasi tutafanya hivi mwakani kimkoa. Lakini historia itaandikwa kuwa tumejifunza Bukombe.

#Serikali ya awamu ya sita inatambua kuwa elimu ndio msingi mkubwa wa maendeleo ambapo mdau mkubwa ni mwalimu.

#Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kuboresha maslahi ya watumishi na hasa walimu ambapo amepandisha vyeo kwa walimu kwa 75% jambo ambalo halikufanyika kwa miaka mingi huku zoezi la kupandisha mishahara likiendelea kufanyiwa kazi.

#Pia ameendelea kuboresha mazingira ya kufundishia ikiwa ni pamoja na kuendelea kujenga madarasa, maabara, vyoo pamoja na mabweni. Sambamba na hili, ajira za walimu zinaendelea kutolewa

#Naomba tuchukue chanjo ya UVIKO 19 ili tukabili gonjwa hili la Korona na chanjo hii ni hiari lakini ni muhimu sana kwetu.

#Nawakaribisha sana kwenye tukio la kuzima Mwenge wa Uhuru katika mkoa wetu ambalo litafanyika Wilaya ya Chato na tunataraji Mgeni Rasmi kuwa Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan.

*MBUNGE WA JIMBO LA BUKOMBE NA WAZIRI WA MADINI: MH DKT.DOTO BITEKO* 

#Nachukua nafasi hii kwanza kabisa kumshukuru Mungu aliyetukutanisha hapa leo tukiwa na afya njema kusherehekea siku hii muhimu kwetu. Walimu wa Bukombe mmenipa heshima kubwa nami nawapenda sana.

#Asanteni sana Walimu wa Bukombe kwa kuja maana mngeamua kutokuja lkn mmekuja. Mnaendelea kunipa deni kubwa sana nami nitaendelea kushirikiana nanyi.

#Hakuna Taifa linaweza kuendelea Duniani bila walimu maana ndo wakiamua kuwafundisha watoto kufanya kazi watafanya.

#Nachukua nafasi hii kumshukuru Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutatua kero za watumishi na hasa walimu.

#Leo nachukua nafasi hii kuwaleta kwenu walimu walionifundisha hadi kufikia hapa nilipo. Asanteni sana walimu wangu na leo nitatoa zawadi ndogo kwenu.

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WALIMU (CWT): BWANA DEUS SEIF.

#Tunampongeza sana Mheshimiwa Biteko kwa kuendelea kuwakusanya walimu Bukombe.

#Sisi kama chama tumeendelea kushughulikia changamoto za walimu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha madeni ya walimu yanaendelea kulipwa ambapo serikali kila mwezi inalipa.

#Tulipambana kuhakikisha Serikali inalipa posho ya madaraka kwa walimu wakuu na wakuu wa shule

#Tumepeleka maombi serikalini kuondoa ukomo wa madaraja kwa walimu kama ilivyokuwa hapo awali.

#CWT tumejipanga kuendeleza walimu wa Sayansi.

#Tumeanzisha Benki ya Mwalimu ambapo mikopo inatolewa kwa watumishi. Hatujawa na matawi mengi lakini tunaendelea kuyafungua.

#CWT italeta Fedha Tsh. Milioni 10 kuchangia ujenzi wa ofisi ya Wilaya unaoendelea.

MBUNGE WA MBOGWE: MH NICODEMAS MAGANGA.

#Nawapongeza sana walimu maana bila walimu tusingekuwa hapa.

#Nampongeza sana Mheshimiwa Biteko kwa jambo kubwa hili maana mwezi juzi tulikuwa hapa kwa ajili ya Doto Cup na leo tupo kwa ajili ya Mwalimu Doto Cup. Mheshimiwa Biteko, Mungu akulipe

Akizungumzia baadhi ya changamoto zinazowakabili walimu, Mwalimu John Lukiko ambaye ni M/Kiti CWT(W) Bukombe amesema kuwa Walimu wanaomba kuwepo kwa usawa katika madaraja kati ya Bukombe na maeneo mengine, walimu wahamishwe na wasikae maeneo yao kwa muda mrefu bila kusahau maslahi yao.

#KusemaNaKutenda

#Kaziiendelee

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge

Jimbo la Bukombe.






Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa