• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Tokomeza ukatili Sasa kwa Wanawake na Watoto

Imewekwa: May 25th, 2018

Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wamepewa mafunzo ya namna ya kutekeleza majukumu yao leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe na wawezeshaji kutoka Mkoani Geita, wakishirikiana na John Snow Inc(JSI), katika mafunzo hayo Kamati hii imefundishwa namna ya kutoa Elimu ya fursa sawa kijinsia, malezi bora ya Mtoto, kumkinga Mtoto na Mwanamke dcidi ya Ukatili, Umuhimu wa Ulinzi na Usalama kwa Mtoto, athari za ukatili ambazo zinaathiri sana Wanawake na Watoto, Kamati hizi katika kila Halmashauri zinalenga kutokomeza kabisa ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kuanzia ngazi ya Kaya, Kijiji, hadi kufika ngazi ya Taifa kupitia Kamati hizi zinazoanzishwa.

Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Kuimarisha Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii katika Halmashauri 84 Tanzania Bara na Visiwani (JOHN SNOW INC(JSI), baad ya kuona matukio ya Kikatili kwa Watoto na Wanawake kutokana na kukosa malezi bora ya wazazi,umaskini,mila na desturĂ­ potofu, tamaa na mabadiliko ya Kiteknolojia, kukithiri hapa nchini. Katika mpango huu wa Taifa wa kutokomeza matukio ya kikatili kwa Wanawake na Watoto, Mkoa wa Geita Halmashauri tatu zitafikiwa, "ya kwanza ni Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, Halmashauri ya Wilaya ya Geita pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Chato ambapo wawezeshaji wawili, Afisa Maendeleo ya Jamii Ndugu Eliana Haroni na Afisa Ustawi wa Jamii Ndugu Frank Moshi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita ,na Msimamizi wa mafunzo haya kutoka JSI ndugu Joseph Bukula watatoa mafunzo haya" alisema Bukula

Ndugu Joseph Bukula amesema kazi kuu wanazofanya JSI ni Kujengea uwezo mabaraza ya WAVIU - KONGA na asasi za kiraia,  Kuimarisha kamati shirikishi za kudhibit UKIMWI (Multi-sectoral AIDS committees), kuanzisha na kujengea uwezo kamati za MTAKUWA,  kushirikiana na Serikali Kuu kuandaa miongozo mbalimbal ya sekta ya afya ya jamii na ustawi wa jamii.

Bukombe ni moja Kati ya Halmashauri 84 zenye ukatili wa Watoto na Wanawake, kwa mujibu wa maelezo ya Afisa Ustawi Ndugu Frank Kasege mpaka sasa jumla ya Kesi 5 za ukatili wa Kimwili, Kesi 20 za ukatili wa Kimapenzi(Mimba za Utotoni) na Kesi 5 za ukatili wa kiuchumi ajira hatarishi kwa watoto. Mafunzo haya yaliyohusisha wadau mbalimbali yatasaidia sana kupunguza au kutokomeza kabisa matukio ya kikatili dhidi ya Watoto na Wanawake ambayo yameonyesha kukithiri sana nchini.

Vikundi vya Kamati ya utekelezaji wa mango wa taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Mtoto na Mwanamke wakiwa kwenye majadiliano.

Vikundi vya Kamati ya utekelezaji wa mango wa taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Mtoto na Mwanamke wakiwa kwenye majadiliano.

Muwasilishaji Bi Josephine wa Kundi Namba 1 akiwa anatoa ufafanuzi wa Majibu ya Swali waliloulizwa katika Makundi.

Msimamizi wa mafunzo kutoka JSI ndugu Joseph Bukula akitoa mafunzo ya Ngazi za kusikiliza Mashauri ya kesi za Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa