• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Tutaleta Umeme Vijijini-Dkt. Biteko

Imewekwa: September 26th, 2023

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema shauku ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona kila Mtanzania anapata umeme bila kujali aina ya nyumba aliyonayo, kwani kila Mtanzania anahitaji mwanga.

Mhe. Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 26, 2023 wakati wa hafla ya uwashaji umeme kupitia Mradi wa REA Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Pili katika Kijiji cha Ihako kilichopo Kata ya Katome, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

“Tutaleta umeme vijijini, hata kama wananchi hawana nyumba nzuri wanahitaji mwanga, hata kama wana nyumba za nyasi  ambazo hazina tarazo wanahitaji mwanga. Watakapopata umeme watapata shauku ya kujenga nyumba nzuri,” amesema Mhe. Dkt. Biteko.

Amesema Serikali imeanza kusambaza umeme katika ngazi ya vijiji, na baada ya vijiji vyote kupata umeme itashuka katika vitongoji.

Aidha, ameiagiza REA kwenda vijijini na kuzungumza na wananchi ili kujua changamoto zao na kuzitatua,

“Nendeni kwa wananchi, nendeni vijijini zungumzeni na wanavijiji, tukaongee lugha zao, tunataka kuona shughuli za REA zikifanyika vijijini na sio mjini, kazi kubwa ya REA ni kupeleka umeme vijijini na sio mijini, hivyo tunataka kuwaona kazi zenu mkifanyia vijijini,” amesema Mhe. Dkt. Biteko.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amesema mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili unalenga kupeleka umeme katika vijiji vyote ambavyo awali havikuwa na umeme, ambapo katika Mkoa wa Geita vijiji 62 na vitongoji vikubwa 65 vitapatiwa umeme kupitia mradi huo, hivyo kufanya jumla ya vijiji/vitongoji vitakavyopatiwa umeme kupitia mradi huu kuwa 127.

“Mkoa wa Geita una jumla ya vijiji 461 ambapo vijiji 399 sawa na asilimia 86.6 vimepata huduma ya umeme kupitia miradi ya awali ikiwemo REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza, REA Awamu ya Pili na REA Awamu ya Kwanza. 

Wakala wa Nishati vijijini umeendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika mkoa wa Geita ikiwa na lengo la kuwapatia huduma za Nishati kwa wananchi ili kuboresha huduma za jamii na kuimarisha shughuli za kiuchumi,”


Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC MURAGILI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE ROBO YA TATU (Januari-Machi 2024/2025)

    May 08, 2025
  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkutano wa baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya 3 kwa mwaka 2024/2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa