• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

USAID boresha Afya kunufaisha wana Bukombe

Imewekwa: September 4th, 2018

Wananchi wilayani Bukombe kunufaika na mradi wa boresha Afya utakaodumu miaka 5, mradi huu umeanza 2017 na utarajiwa kuisha 2021, mradi huu wenye lengo la kuboresha huduma za Afya zinazotolewa na wahudumu wa afya katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospital za wilaya kwa wamama wajawazito na watoto kutokana na changamoto kubwa zinazowakabili wa mama hao.

Mkuu wa wilaya ya Bukombe Mhe. Said Nkumba, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Safari Mayala, Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na maji Mhe.Leokadia Kasase pamoja na watoa huduma ya afya ya uzazi na mtoto wamepewa elimu ya kutoa  huduma zenye utu, heshima na staha zinazozingatia usawa kijinsia wakati  wa ujauzito, kujifungua na kunyonyesha.

Katika semina hiyo ya boresha afya, watoa huduma wameelimishwa kila Mwanamke, Mtoto na kijana wanayo haki ya kupata huduma za afya zenye ubora na  viwango stahiki kwa kadiri iwezekanavyo kwa kuzingatia haki, staha na utu wa Mwanamke ili kulinda afya ya mama na mtoto, pia ili kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto ni lazima jamii iache ukatili wa kimwili,kingono kiuchumi na ukatili wa kihisia na kiakili mfano lugha chafu na ya kudharirisha kushindwa kupata huduma yenye ubora na ya kitaalamu. 

Akizungumza katika semina hiyo mratibu wa afya ya uzazi na mtoto wa wilaya Ndugu Masanja Nkolla amesema huduma ya afya na uzazi wa mpango ikiwa bora itapunguza vifo vya wazazi na watoto kwa kutengeneza mpango mkakati  wa mawasiliano kituoni ambapo kutakuwa na simu ya kituo cha afya ili kutoa taarifa kwa haraka, aidha huduma ya uzazi wa mpango ipo chini lakini kupitia USAID boresha afya watasaidia kuwezesha huduma kwa kutoa mafuta kwenye vituo ili wahudumu kuweza kufikia sehemu ambazo hazifikiki kwa urahisi, watanufaika na vifaa tiba , machine za kupumulia watoto na msaada wa kitaalamu, pia huduma ya mikoba itaboreshwa zaidi  kupitia mradi huu.   

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe Mhe. Safari Mayala naye amesema wahudumu wa afya washirikishe waheshimiwa madiwani pale wanapotembelea kata au vijiji husika ili waweze kufanya na kamati za maendeleo  ya vijiji ili kutoa elimu hii ya afya ya uzazi na mtoto ambayo itaokoa maisha ya mama na mtoto, na amesema siku ya mkutano wa baraza atamualika mtoa huduma mmoja ili aweze kutoa elimu ya afya ya uzazi na mtoto kwa waheshimiwa madiwani ambao ni wawakilishi wa wananchi

Mkuu wa wilaya Mhe. Said J Nkumba katika semina hiyo amewataka watumishi wa afya kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia huduma yenye staha na utu, pia amewaonya kuacha vitendo vya rushwa ambavyo vinafifisha huduma bora kwa wananchi, sambamba na hilo amesema atakuwa anaongozana na wahudumu wa afya katika mikutano ya hadhara ili kutoa elimu ya afya ya uzazi na mtoto ili kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao hawahudhuri klinki,wanachelewa kufika katika vituo vya afya hali ambayo hupelekea vifo kwa watoto au mama kupata ugonjwa wa fistula.

Mkuu wa wilaya ya Bukombe mhe. Said Nkumba akichangia jambo katika semina ya boresha afya siku ya kwanza.

Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bukombe mhe. Said Nkumba, katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe mhe.Safari Mayala katika kazi ya kundi kuhusu boresha afya siku ya pili. 

 

                                                                          Washiriki mbalimbali katika  Mafunzo ya boresha afya.

 Washiriki ambao ni wahudumu wa afya katika makundi  kuandaa mpango kazi wa Mafunzo ya boresha afya.

 Washiriki ambao ni wahudumu wa afya katika makundi  kuandaa mpango kazi wa Mafunzo ya boresha afya.


 Muuguzi Mwandamizi Agness Kessi na Katibu wa Afya Mayasa  katika makundi  kuandaa mpango kazi wa Mafunzo ya boresha afya.

Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto wilaya Masanja Nkolla kushoto akiwa na Sheikh wakiandaa mpango kazi kwa makundi.

Miongoni mwa washiriki katika semina ya boresha afya Bi. Agness Kessi ambaye ni Muuguzi Hospital ya wilaya.

Relocates Kadoshi mwezeshaji  kutoka USAID Boresha afya ailpokuwa akichangia majadiliano.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa