• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Vyakula Viwekewe Virutubisho Muhimu

Imewekwa: October 27th, 2022

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Ndg. Lutengano Mwalwiba amezitaka shule zote zinazopokea ruzuku ya chakula kutoka serikalini kuhakikisha  vyakula hivyo  vinawekewa virutubisho muhimu vyenye mchanganyiko wa  madini ya chuma, zinki, vitamin B12 pamoja na asidi ya foliki.

" Tuhakikishe vyakula vya watoto wetu mashuleni vinakuwa na virutubisho  muhimu ili watoto wetu waweze kupata lishe bora pamoja na kuongeza ufaulu."

Vile vile ameziagiza shule binafsi zinazotoa huduma ya chakula kuhakikisha  zinatekeleza agizo  hilo.

Agizo hilo amelitoa  tarehe 26 Oktoba, 2022 wakati wa kikao cha kamati ya lishe cha Wilaya kwa kipindi cha robo mwaka ya kwanza (Julai hadi Septemba, 2022)

Akiwasilisha taarifa ya zoezi la utoaji wa Vitamini A na dawa za minyoo kwenye mwezi wa afya na lishe ya mtoto Afisa lishe Wilaya  Ndg. Said Athumani Ally amesema, Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe  kupitia Idara ya Afya imetekeleza zoezi la mwezi wa afya na lishe ya mtoto kwa kuwapatia dawa za minyoo na  vitamin A  watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

.Kwa upande wake  Mratibu wa Mashauri ya Watoto katika Mradi wa ACHIEVE kutoka Shirika la NELICO kwa kushirikiana na Pact  Tanzania amesema wataendelea kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe katika kuboresha huduma za lishe ili kuwasaidia watoto walioathirika na Virusi Vya  Ukimwi kuwaboreshea huduma za elimu, Lishe na Uchumi.

Naye Mganga Mkuu Wilaya Dr. Deograsia Mkapa amesema  mpaka sasa Watendaji wa Kata 17 wameishasaini mikataba ya lishe na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ili kuhakikisha watoto wote chini ya umri wa miaka mitano wanapata lishe bora yenye virutubisho muhimu katika siku 1000 za awali za makuzi ya mtoto.

Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe  imefanikiwa kuwafikia watoto 65,408 wenye umri kuanzia miezi 6 hadi 59 ambao wamepata matone ya myongeza ya vitamini A sawa na asilimia 108 ya malengo ya watoto 60,588 waliotakiwa kufikiwa.

MWISHO

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa