• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mkakati ni Kuondoa Ziro na Kupunguza Ufaulu wa Daraja la Nne

Imewekwa: February 2nd, 2022

"Mkakati ni Kuondoa ziro na kupunguza ufaulu wa Daraja la nne katika shule zetu za sekondari."Mhe.Yusuph.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mhe. Yusuph Mohamed Yusuph amewataka Wakuu wa shule kuhakikisha wanaweka mkakati wa kuondoa ziro na kupunguza ufaulu wa Daraja la nne katika matokea ya mtihani wa Taifa kidato cha nne na sita kwa lengo la kuongeza ufaulu wa wanafunzi kuanzia daraja la tatu hadi la kwanza.

" Ufaulu wa kidato cha nne na kidato cha sita tunategemeana walimu wa shule za Msingi na sekondari.Tukiweka nia inawezekana kabisa kuondoa ziro katika matokeo ya kidato cha nne na kidato cha sita.

Aidha amesema kuwa shukrani pekee ya kumpa Rais wetu katika madarasa haya ya UVIKO - 19 ni kuhakikisha tunafundisha kwa bidii na watoto wanafaulu."

Hayo ameyasema tarehe 1 Februri, 2022 wakati wa ziara ya kamati Fedha Uongozi na Mipango ilipotembelea miradi inayotekelezwa chini ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO - 19 ambayo ni ujenzi wa vyumba vya madarasa kumi katika shule shikizi Idoselo, vyumba sita vya madarasa katika shule ya sekondari Namonge, vyumba viwili vya madarasa katika shule shikizi Mkange, chumba kimoja cha darasa katika shule ya sekondari Iyogelo na vyumba vinne vya madarasa katika shule ya sekondari Busonge.

Aidha amewapongeza walimu kwa ufaulu mzuri wa matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2021.

"Hongereni walimu kwa ufahulu mzuri wa matokeo ya kidato cha nne kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa.Asanteni kwa kazi nzuri."

Akiongea katika ziara hiyo Fundi Sanifu Majengo Neema Makala amewataka Wakuu wa Shule na walimu wakuu kuhakikisha wanaomba idhini ya kutumia  fedha pamoja na vifaa vilivyobaki wakati wa ujenzi wa miradi ili viweze/ziweze kutumika katika miradi mingine.

Akiongea katika mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Bufanka kinachotekelezwa na fedha ya Tozo ya Mawasiliano kiasi cha shilingi Milioni 250 Mhe. Yusuph amemtaka Mganga Mkuu wa Kituo hicho kuhakikisha anaongeza idadi ya mafundi ili kituo kiweze kukamilika kwa wakati na kiweze kutoa huduma kwa wananchi.

Naye Mganga Mkuu wa Kituo hicho Winifrida Daudi amesema kwa kipindi cha mwezi Disemba, 2021 miundombinu ya barabara iliharibika na kupelekea magari ya kubeba vifaa vya ujenzi kushindwa kufika eneo la mradi.

Mradi mwingine wa afya uliotembelewa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha Afya Namonge kilichopokea kiasi cha shilingi Milioni 400 kutoka Mfuko wa Afya wa Pamoja na kipo katika hatua ya umaliziaji.








Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa