• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi wapongezwa kwa kushiriki shughuli za maendeleo

Imewekwa: January 16th, 2019

Mhe. Rozalia Masokole  Diwani wa kata ya Bukombe kwa niaba ya Mwenyekiti wa kamati ya Elimu, Afya na Maji amewapongeza Wananchi wa Wilaya ya Bukombe kwa ushirikiano wao mzuri na viongozi katika kushiriki na kusimamia miradi ya maendeleo .”Hongereni sana wananchi kwa ushirikiano wenu mzuri mnaounyesha kwa viongozi wenu katika kuibua na kushiriki ujenzi wa miundombinu ya madarasa, afya na maji”

Pongezi hizo amezitoa wakati kamati ya Elimu Afya na Maji ilipofanya ziara ya  kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo tarehe 15 – 16/01/2019 lengo likiwa ni kuhakikisha miradi hiyo inajengwa kwa kiwango kilichokusudiwa na kukamilika kwa wakati.

Aidha Mhe. Rozalia amewaomba wananchi kuhakikisha wanaendelea kujitolea katika kuchangia shughuli za maendeleo hasa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi wa kidato cha kwanza walionza masomo tarehe 07 Januari,2019.

Naye Mhe. Erick Kagoma Diwani wa Kata ya Bulega alisema kituo cha Afya Bulega kilipokea jumla ya Milioni 124 kutoka mfuko wa pamoja wa afya (Health Basket Fund) fedha hiyo ikiwa ni kwa ajili ya ujenzi wa Maabara, ununuzi wa vifaa tiba pamoja na utengenezaji wa mfumo wa maji. Pia amewaahidi wanakamati kuwa kufikia mwishoni mwa mwezi  Februari 2019 ujenzi wa jengo la Maabara kituo cha Afya Bulega utakuwa umekamilika

Aidha Mhe. Yusuph Mohamed  Diwani wa Kata ya Bulangwa amemuagiza Mkuu wa shule  ya sekondari Busonzo Ndg. Simeo Naluyaga kuhakikisha anatambua na kuweka mipaka eneo lote la shule kwa kushirikiana na wananchi ili kuepusha uvamizi holela wa ardhi katika eneo hilo.

Pia Amemuagiza Afisa elimu sekondari ndg Philbert Nyangahondi kuhakikisha anaweka kwenye bajeti  ya mwaka 2019/2020 ununuzi wa miundombinu ya uvunaji wa maji ili kukabiliana na changamoto ya maji inayowakabili walimu pamoja na wanafunzi wa shule hiyo.

Miradi iliyotemelewa ni pamoja na upanuzi wa mradi wa maji Bulangwa, ukamilishaji wa Zahanati ya Businda, ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa shule tarajali Kidete, ukarabati wa madarasa shule ya sekondari Bukombe, ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa na ofisi 1 shule ya msingi Nyikonga, ujenzi wa Maabara kituo cha afya Bulega, ukamilishaji wa OPD kitu cha afya Msonga, ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa na ofisi 2 shule ya msingi Kasozi, ujenzi wa vyumba 2 na ofisi 1  shule mpya Kelesia pamoja na kutembelea shule ya sekondari Ushirombo, Busonzo na shule ya msingi Azimio.


Ujenzi wa Maabara  kituo cha afya Bulega  


    Ujenzi wa vyuma vitatu vya madarasa na ofisi moja  shule ya msingi Nyikonga


Mhe. Yusuph Mohamed  Diwani wa Kata ya Bulangwa (katikati) akitoa taarifa ya ujenzi wa Maabara  kituo cha Afya  Bulega.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa