• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Bomba la mafuta kunufaisha wananchi wa Bukombe

Imewekwa: March 20th, 2018

Wananchi wa wilaya ya Bukombe wanatarajia kupata fursa za ajira za muda mrefu na mfupi, pamoja na wakulima wanaozalisha mazao mbalimbali hasa ya chakula kufanya biashara, kutokana na ujenzi wa  kambi ya wajenzi wa bomba la mafuta kutoka Ohima, Uganda kwenda Tanga, Tanzania hivi karibuni.

Ujenzi wa kambi hiyo ya kudumu wilaya ya Bukombe licha ya kuongeza kipato kwa wananchi na Taifa kwa ujumla, pia itapandisha zaidi hadhi ya wilaya ya Bukombe kutokana na uwepo wa wafanyakazi zaidi ya elfu moja kutoka katika nchi za Uganda, Tanzania na nchi nyingine ambazo zitaleta wataalamu wa masuala ya ujenzi wa bomba la mafuta.

Wananchi wa maeneo mbalimbali wilayani Bukombe wameelezea kufurahishwa na mradi huu ambao utasaidia kukuza uchumi wa wilaya, na kuongeza miundombinu mbalimbali hasa ya barabara na kufanya wilaya ya Bukombe kujulikana kitaifa na kimataifa kwakuwa itakuwa kambi hiyo yenye watu kutoka mataifa mbalimbali ambao watakuwa wateja wa biashara na huduma wanazozitoa.

Bi.Mariam Abell kutoka kijiji cha Bukombe amesema uwepo wa mradi huu kwake imekuwa faraja “hawa wataalamu wametushirikisa kila hatua ya utambuzi wa nani mmiliki halali wa maeneo haya  kwa uwazi, pia najiandaa kuwa mama ntilie ili nipike wakati  wa ujenzi wa kambi hii,alisema Bi.Mariam

Wakati huo huo wataalamu mbambali wanaosimamia mradi huu kwa kushirikiana na wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri  wamebainisha eneo la Hekta 17 lililopo mkabala na mnada mkubwa wa Bukombe, kijiji cha Bukombe kitongoji cha Isambala ambalo litatumika katika ujenzi wa kambi ya wajenzi wa bomba la mafuta. Zoezi la utambuzi kwa wamiliki halali wa maeneo hayo na mali zao umefanyika ili wananchi waweze kulipwa fidia stahiki.

Mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki umeanzishwa baada ya ugunduzi wa mafuta mnamo mwaka 2006, na yatazalishwa katika bonde la ziwa Albert nchini Uganda, ujenzi wa boma hili la mafuta lenye urefu wa kilomita 1,450 chini ya ardhi litasafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda kwenda pwani ya bahari ya Hindi ili kulenga masoko ya kimaifa, ujenzi huu utadumu zaidi ya miaka miwili.


 

 Wananchi wa kijiji cha Isambala kata ya Bukombe wakionyesha nyuso za unufaikaji wa mardi wa bomba la mafuta baada ya utambuzi wa maeneo yao.


  Bi.Mariam Abell akiwa ameshikiria bango la taarifa zake zitakazotunzwa kama kumbukumbu baada ya zoezi la utambuzi wa eneo lake litakalochukuliwa na mradi.


 Mtaalamu wa Ardhi Bwana Francis akimpiga picha Mzee Kasandiko ili kutunza kumbukumbu ya mmiliki halali wa Eneo Hilo wakati wa kulipa fidia stahiki kusiwepo udanganyifu.

 Alama ya kipande cha mti chenye kibendera zilizowekwa katika maeneo ya ujenzi wa mradi wa kambi ya wajenzi.


 Makazi ya wananchi yatakayochukuliwa kupisha ujenzi wa mradi huu.


Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC MURAGILI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE ROBO YA TATU (Januari-Machi 2024/2025)

    May 08, 2025
  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkutano wa baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya 3 kwa mwaka 2024/2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa