• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WANAWAKE BUKOMBE WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUPIMA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI NA MATITI

Imewekwa: March 1st, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Said Nkumba amewataka wanawake wote katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kujitokeza kwa wingi kufanya uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi pamoja na Matiti.

Nkumba ameyasema hayo leo tarehe 01 March, 2024 wakati wa  zoezi la upimaji wa Saratani ya Shingo ya Kizazi na Matiti katika Hospitali ya wilaya ya Bukombe ikiwa ni shughuli kuelekea kilele cha Siku ya Mwanamke Duniani yenye kauli mbiu isemayo "Wekeza kwa Wanawake, Kurahisisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii."

Aidha Nkumba amewataka wanawake kufanya uchunguzi ili kujua hali zao.

“Jitokezeni kwa wingi ili  mfanye uchunguzi mapema na muweze kujua hali za afya zenu na muweze kupata matibabu kwa haraka zaidi”

Vile vile Nkumba aliongeza kwa kusema kuwa Saratani inauwa sana kwasababu watu wengi hawana utaratibu wa kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Lutengano Mwalwiba, ameipongeza Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Idara ya Afya kwa kuratibu zoezi hilo kwani litasaidia wanawake wengi kujua afya zao. 

 “Hongereni sana kwa kuwa chachu ya Maendeleo katika jamii kwa kujali na kuthamini afya za wanawake wote kwani afya ni mtaji”.

Naye  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Bukombe Dr. Yohana Fumbuka akiongea kwa niaba ya Mganga mkuu wa Wilaya ya Bukombe, amewataka wanawake kuwa na utaratibu wa kufika hospitali mara kwa mara kwa ajili ya kufanya uchunguzi kwasababu Saratani ikigundulika kwa haraka inakuwa rahisi kutibika na kuokoa uhai wa wanawake wengi.

Zoezi la upimaji wa Saratani ya Shingo ya Kizazi na Matiti linafanyika bure kuanzia tarehe 01-05 March 2024 ikiwa ni muendelezo wa matukio mbalimbali yatakayofanyika katika kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani  ambapo katika Wilaya ya Bukombe itafanyika siku ya tarehe 06 March, 2024 katika viwanja vya Stendi ya Mabasi Ushirombo.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa