• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awatangazia neema wanageita Bukombe ikiwemo

Imewekwa: September 30th, 2018

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa wakati akifunga maonesho ya Uzalishaji bora wa Dhahabu leo uwanja wa Kalangalala mkoani Geita amesema Dola Milioni 45 zimetengwa za Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda kwenye wilaya zote za Mkoa wa Geita ikiwemo Wilaya ya Bukombe.

Mhe.Waziri Mkuu amewataka Wachimbaji wadogo kutumia fursa ya Benki kuu ya kutoa mikopo ili waweze kujiendeleza katika shughuli za uchimbaji, "Mnakopesheka, msihofu kukopa" alisema mhe. Kassim Majaliwa, Pia amewataka wakuu wa Wilaya kusimamia uanzishwaji wa vikundi kwa wachimbaji wadogo ili waweze kupata mikopo.                                                     Katika kufunga maonesho hayo Mhe.Kassim Majaliwa amewasihi viongozi Waziri wa Madini na Mkuu wa Mkoa kuendelea kusimamia makampuni ya madini kushirika katika shughuli za kijamii, kama Sheria mpya ya mad ini inavyotaka, na amewasisitia wachimbaji kulipa kodi "wachimbaji lipeni kodi  kwa manufaa  ya  nchi, mabadiliko makubwa katika sekta ya madini yameanza kuonekana, zile kero nyingi katika sekta hii zimeanza kuondoka na tutafika mahali tunapotaka, ifikapo 2025 malengo yetu katika sekta ya mad ini tune tumeyatimiza". alisema Waziri Mkuu.


Aidha Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ifuatilie wachimbaji wakubwa wenye leseni za maeneo ya mad ini na hawayaendelezi, na washughulike nao, semrikali itajenga  vituo vya afya kila panapowezekana, kwasasa kuna vituo vya afya 345 ambapo itaendelea na awamu ya tatu na nne, mpaka kufika 2020 mambo yatakuwa mazuri.
Aidha mhe.Kassim Majolica amesisitiza viongozi wanaosimamia miradi hiyo ya afya kutogusa fedha hizo mbali kutekeleza miradi hiyo kwa uhakika na makini "fedha za Serikali zina moto msiziguse, zitawaunguza, hizo ni kwa ajilli ya kuwahudumia wananchi" alisema Waziri Mkuu, Pia amezitaka taasisi za kibenki kuweka utaratibu wa kununua dhahabu kwa wachimbaji wadogo ili kuwasaidia.

Naye Waziri wa Madini Mhe. Angela Kairuki amesema kuwa ifikapo 2025  sekta ya madini ichangia pato la taifa kwa asilimia isiyopungua 10, serikali imechukua hatua ya kuzuia kusafirisha Kaboni (Carbon) nje ya mkoa inapopatikana  hali ambayo imesaidia sana mkoa wa Geita pamoja na wachimbaji wadogo.  Pia Mhe.Waziri wa Madini amewataka viongozi wote kusimamia makampuni ya madini kutoa sehemu ya faida zio kama uwajibikaji wa kampuni kwa jamii ili kuendeleza huduma muhimu kwa jamii. Aidha Waziri wa madini ameiagiza kampuni ya uchimbaji madini GGM kulipa wananchi fidia " kamati niliyoiunda kuchunguza athari za mitetemo katika migodi, imeniletea ripoti na imeonesha shughuli za uchimbaji zina athari, hivyo naagiza ikifika tarehe 24/10/18 kampuni ya GGM ikae na wananchi ili waweke utaratibu wa kuwalipa" alisema Mhe.Agela Kairuki.

Pia Waziri wa Madini Mhe.Angela Kairuki amesema Bukombe kutajengwa kituo cha mfano cha uchejuaji katika hafla ya  kufunga maonesho ya Teknolojia ya uzalishaji bora wa dhahabu kwa maendeleo ya kijamii na uchumi wa Viwanda yaliyofanyika Mkoani Geita uwanja wa Kalangalala.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amesema kwa muda mrefu Moka wa Geita umekuwa ukihujumiwa katika sekta ya mad ini, nawaahidi wanageita nitasimamia rasilimali hii kwa nguvu zangu zote ili ziwanufaishe wanageita na mabadiliko ya Sheria ya mad ini yametuwezesha kushirikiana na makampuni ya mad ini kwa asilimia 100 katika kuimarisha huduma za jamii ikiwamo vituo vyg)ffça afya na katika sekta ya elimu.

Wanafunzi kutoka wilaya ya Bukombe watumbuiza Maonesho ya Kihistoria ya Uzalishaji Dhahabu kwa Maendeleo ya Kijamii na Uchumi wa Viwanda yaliyofanyika Mkoa wa Geita Uwanja wa CCM Kalangalala na kujizolea umaarufu mkubwa baada ya kuimba Nyimbo yenye maudhui mazuri ya kusifia Mkoa wa Geita na Rasilimali zake nzuri zilizobarikiwa na Mungu mbele ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alipokuwa akifunga maonesho hayo. "Madini ya Dhahabu, Uwepo wa Ziwa Victoria, Ufugaji Nyuki ambao unatokana na uwepo wa hifadhi ya misitu, Kilimo cha uhakika Mihogo,Mpunga,Mahindi,Pamba, Hifadhi ya wanyama Rubondo, na mengi ya kupendeza mkoani Geita".



Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC MURAGILI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE ROBO YA TATU (Januari-Machi 2024/2025)

    May 08, 2025
  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkutano wa baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya 3 kwa mwaka 2024/2025
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa