• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Waziri Mkuu Majaliwa aagiza maonesho ya madini Geita yafanyike kitaifa.

Imewekwa: September 22nd, 2021

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza Maonesho ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita kila mwaka kuwa ya kitaifa huku akitaka miundombinu katika maonesho hayo kubeba sura ya Kimataifa ili Geita itambulike kuwa Kitovu cha Dhahabu duniani.

Ametoa maagizo hayo, leo tarehe 22 Septemba 2021 wakati akifungua rasmi Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Kituo cha Uwekezaji cha Bombambili , Geita.

Akizungumza umuhimu wa maonesho Waziri Mkuu Majaliwa ameeleza, maonesho yamekuwa na manufaa makubwa katika kuhamasisha wananchi kujihusisha na shughuli za madini nchini ikiwemo kuwaweka karibu wachimbaji wadogo katika kutangaza fursa zilizopo katika Sekta ya Madini kwa manufaa ya Geita na Taifa.

"Manufaa hayo, tumeanza kuyashuhudia kwa migodi mingi kuanza kutumia huduma na bidhaa zinazozalishwa nchini kutoka kampuni za wazawa.

 Pia idadi ya Watanzania wanaoshiriki na kunufaika na uwepo wa rasilimali hizi imeongezeka," amesema Waziri Mkuu.

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amesema, Sekta ya Madini imeendelea kutoa mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa na maendeleo ya mtu mmoja mmoja nchini. Amesema matarajio ya Serikali ni kuongeza zaidi mchango huo kupitia Shughuli za uchimbaji, uchenjuaji, usafishaji madini, usanifu madini na utoaji wa huduma katika shughuli za madini.

Akieleza changamoto za wachimbaji wadogo, amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri ya kusaidia wachimbaji wadogo kufikia malengo yao.

"Serikali imeweka mikakati ya kuimarisha Taasisi zake hususan Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na STAMICO ili taasisi hizo ziweze kutoa huduma bora na nafuu kwa wachimbaji wadogo," ameongeza Waziri Mkuu Majaliwa.

Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu Majaliwa ameagiza Wizara ya Madini kuhakikisha suala la Local Content linasimamiwa kikamilifu. Aidha amesisitiza kutumia CSR kama chachu ya kuleta maendeleo yenye tija kwa kizazi cha sasa na baadaye kwenye Halmashauri zote.

Naye, Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema, mafanikio yote yanayopatikana kwenye Sekta ya Madini, ni kwa sababu ya usimamizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

"Mhe. Rasi Samia alitoa maelekezo mahususi kwa Wizara na Taasisi zake, ya kwanza nendeni kuwasikiliza wachimbaji wadogo, wa Kati na Wakubwa," ameeleza Dkt. Biteko.

Aidha, Dkt Biteko ameeleza kuwa, toka amepata maelekezo hayo mambo makubwa yamefanyika kwenye wizara na migodi mikubwa ambayo inaendesha shughuli za uchimbaji.

Akieleza kuhusu Sheria ya Local Content Dkt. Biteko ameeleza kuwa, Wizara imetoa maelekezo Maalum kuwa Local Content lazima itekelezwe. Amesema kazi kubwa ya kuchoronga inayokuja kwa Kampuni ya GGML ambayo inathamani ya Dola za Marekani Milioni 183 lazima Mgodi huo uungane na Kampuni za ndani.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule amesema Mkoa wa Geita unaongoza kwa uchimbaji na upatikanaji wa madini ya Dhahabu.

 Amesema kuwa zaidi ya asilimi 40 ya Dhahabu inayouzwa hapa nchini inapatikana katika mkoa wa Geita.

Maonesho ya Madini yaliyofunguliwa rasmi leo yalianza tarehe 16 Septemba yanatarajia kufungwa tarehe 26 Septemba 2021.

Ufunguzi wa maonesho yamehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Wabunge na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini.






Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa