• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Yaliyojiri leo tarehe 4/9/2021.

Imewekwa: September 5th, 2021

Kufunga Tamasha la Ligi ya Doto cup 2021 Wilayani Bukombe.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO MHE. INNOCENT BASHUNGWA (MB).

#Namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ameniwezesha kufika Bukombe kwenye viwanja vya shule ya sekondari Ushirombo.

#Pamoja na wajumbe nilioambatana nao tunawashukuru kwa mapokezi yenu mazuri asanteni sana.

#Hapa Bukombe kweli mpira upo.

#Leo nimejionea mwenyewe pamoja na Wabunge ambao tupo hapa.

#Kwa kweli hapa vipaji vipo. Hongereni sana.

#Ninakupongeza sana Mhe.Biteko kwani kuna msemo usemao ukiona vyaelea ujue vimeundwa.

#Wewe ndiye uliyesaidia kuviunda vipaji hivi na kuvitengenezea mazingira wezeshi na kuhakikisha kila mwaka kunakuwa na Ligi inayoitwa Doto Cup kutoka mwaka 2016 mpaka hivi sasa.

#Huu ni upendo wa kipekee kwa wanabukombe. Mwenyezi Mungu akubariki sana.

#Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amenipatia maelekezo mahususi ya kuhakikisha tunatambua vipaji kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Tarafa.

#Kuhakikisha tunarudisha uhai wa UMITASHUMITA na UMISETA.

#Kurudisha Taifa Cup ili kuinua vipaji kwenye Mikoa.

#Kwa kazi nzuri unayoifanya ni kuhakikishie kuwa serikali itaendelea kuungana na wewe ili kuendeleza vipaji hivi.

#Kwa kazi nzuri ambayo nimeiona ya maendeleo ya michezo nitawaagiza Chuo Cha Michezo Malya kuweka kituo shikizi hapa.

#Waalimu wa michezo katika shule zetu pamoja na wale wanaotaka kusomea Ukocha na Uamuzi wapate elimu hiyo bila usumbufu wowote.

#Naahidi mifuko 100 ya saruji kama zawadi yangu kwenye mashindano haya.

#Mifuko hii ikajenge Uwanja wa Michezo wa Halmashauri.

#Ili mashindano yajayo yakafungiwe kwenye uwanja wa Halmashauri.

#Serikali inataka kuanzisha shule mahususi za Michezo.

#Kila Mkoa utakuwa na shule ya msingi na sekondari maalumu kwa ajili ya michezo.

#Mkoa wa Geita utanufaika na mpango huu maalumu wa serikali.

#Napenda kuwakumbusha na kuwasisitiza Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya kuwa wao ndiyo wenyeviti wa kamati za michezo.

#Simamieni majukumu yenu.

#Nimalizie kwa kuwapongeza washiriki wote wa mashindano ya Doto Cup.

#Hongereni kwa kushiriki na hongereni washindi wote.

#Napenda kuwakumbusha wanabukombe endeleeni kuchukua taadhari ya ugonjwa wa UVIKO - 19.

#Mimi nimechanja nawahamasisha na nyinyi mkachanje.

#Kuchanja ni hiari lakini mimi nasema kuchanja ni muhimu.

Imetolewa na :-

Kitengo cha TEHAMA

Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

Tarehe 4 Septemba, 2021.





Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa