• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • M.M.M |
    • Barua pepe |
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL
BUKOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Kilimo na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Idara ya Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Mifugo na Uvuvi
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba
      • Ratiba ya Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

zaidi ya bilioni 33.5 zimetumika kama wajibu wa wamiliki leseni kutekeleza miradi kwa jamii

Imewekwa: September 9th, 2022

Wizara yakamilisha Rasmi ya Kanuni za kusimamia Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini*

Imeelezwa kuwa, tangu kufanyika kwa maboresho kwenye Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, zaidi ya shilingi bilioni 33.5 zimetumika katika miradi mbalimbali iliyotekelezwa na wamiliki wa leseni za miradi katika mikoa mbalimbali hapa nchni.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba wakati akiwasilisha taarifa kuhusu mafanikio na changamoto za utoaji na upatikanaji wa huduma kwa jamii kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jijini Dodoma.

Amesema Sheria ya Madini, Sura 123 ilivyofanyiwa maboresho na kuwekewa kifungu cha 105 ambacho kinaelezea utaratibu mzima wa kuandaa na kutekeleza mipango ya wajibu wa Kampuni kwa jamii, suala ambalo limekuwa na mafanikio makubwa ikilinganishwa na kipindi cha nyuma ambapo kampuni zilikuwa zikiwajibika kwa jamii kwa utaratibu wanaojiamulia.

Ameongeza kuwa, kwa mujibu wa Sheria ya Madini, Sura 123, Mmiliki wa Leseni ya Madini analazimika kila mwaka kuandaa Mpango unaoaminika ambao umekubaliwa kwa pamoja na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa kushauriana na Waziri anaye husika na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Waziri anaye husika na masuala ya Fedha ambapo mpango huo utaangazia masuala ya mazingira, kijamii, utamaduni na kiuchumi kwa kutoa kipaumbele kwa jamii inayozunguka mgodi.

Pamoja na mafanikio hayo, Samamba amesema bado kuna changamoto ya uelewa mdogo juu ya wajibu wa kampuni kwa jamii na pia kumekuwepo na utekelezaji hafifu wa miradi kwa baadhi ya Halmashauri.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Wizara ya Madini Godfrey Nyamsenda amesema wizara imekamilisha Rasmi ya Kanuni zitakazo simamia masuala ya Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini kwa Jamii ili kuboresha na kuweka usawa kwenye matokeo ya utekelezaji wa miradi.

Nyamsenda amesema uandaaji wa Rasimu ya hKanuni hiyo umezingatia matakwa ya Sera ya Madini ya Mwaka 2009 ambayo yanaeleza umuhimu wa kuimarisha ushiriki wa jamii katika miradi ya madini na kuhimiza kampuni za madini kuongeza uwajibikaji kwa jamii.

"Kanuni hizi ni muhimu kwa kuwa zinalenga kuondoa mapungufu yaliyokuwepo katika utekelezaji kwenye eneo la wajibu wa wamiliki wa leseni za madini kwa jamii kwa watekelezaji ikiwa ni sehemu ya matakwa ya Sheria ya Madini, Sura 123," amesema Nyamsenda.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema, wizara yake imeona ni sahihi kuwasilisha Rasimu ya Kanuni hiyo ili kupata maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo inasimamia Sekta hiyo.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Adolf Ndunguru ametoa ufafanuzi juu ya Rasimu hiyo na kuahidi kuyafanyia kazi maoni na ushauri uliyotolewa na Wajumbe wa Kamati hiyo.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10 February 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 23, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA 10% October 07, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • DC MURAGILI AHAKIKI TAARIFA ZAKE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 05, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOA WA GEITA.

    May 02, 2025
  • MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAWAKE BUKOMBE WASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI DOTO BITEKO.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mfumo wa Bajeti(Planrep)
  • Mfumo wa Fedha Vituo vya kutoa huduma(FFARS)
  • MTUHA
  • Maktaba ya Picha
  • Ramani ya Bukombe
  • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ushirombo

    Sanduku la Posta: S.L.P 02

    Simu ya Mezani: 028 2520704

    Simu ya mkononi: +255 (0) 622 295619

    Barua Pepe: ded@bukombedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • M.M.M
    • Mpangilo wa Tovuti
    • Service

Hatimiliki(c) 2017 Halmashauri ya Bukombe. Haki zote zimehifadhiwa